Mnaongeleaje wizi wa mafuta sheli, yaani kujaza upepo?

Nawapenda TOTAL hawataki ujinga
 
Kinara wa wizi wa mafuta Tanzania ni OilCom ya barabara ya Kawe karibu na Rainbow
Karibia wote tu. Nilitaka kurusha ngumi pale Tabata- Shule! Unajua uzuri gari kama umelizoea mafuta ya Tsh 20,000 au 30,000 utajua tu yanafika level gani. Sasa ukipunjwa utajua tu
 
Nadhani ni EWURA, japo vipimo wanahusika.
 
-omba risiti.
-angalia mashine ya pump ya mafuta imesoma kiwango ulichotaka.
**wamiliki wa kampuni za mafuta hawatambui wizi huu unaofanywa na wafanyakazi**
Bro hii haisaidiii
Kama ndo unafata hvyo unajidanganya bro
Sio wajinga kias icho
Wanacheza na usayansi wa mashine
 
Dah...siku kilihappen zilipoingia Lita 120 kwenye tank lenye ujazo wa lita 100 lililokuwa robo tank kabla....wadada wa BP walinipenda ghafla...nilipewa mabusu makali...hasira zangu zikatulia[emoji13] [emoji13]
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Kuna cku jini likaniishia mafuta mitaa ya mbezi,nikaomba kidumu kwa jamaa wa boda boda,nilipoenda petrol station na kidumu,nikaaambiwa meneja aruhusu kununua mafuta kwenye kidumu,ikabidi niwe mpole
ulipigwa jamaa, pole sana!
 
Your talking of the impossibles
Kila m2 anamizunguko yake kuliko kufatilia kuwa shtaki wajamaa
Tunachotaka kujua ni kipi kiko poa ili kuepuka na hii ki2 kabla haijakutokea
Kabla ajali haijatokea unatafta njia ya kuiepuka
 
ndio madhara ya kuweka graduates katika petro stesheni afu wanalipwa kama mtoa huduma wa huduma kwa wateja wa kabang
 
Kuna cku jini likaniishia mafuta mitaa ya mbezi,nikaomba kidumu kwa jamaa wa boda boda,nilipoenda petrol station na kidumu,nikaaambiwa meneja aruhusu kununua mafuta kwenye kidumu,ikabidi niwe mpole
Sehemu kama hizo ogopa kama ukoma ni wezi wa nwendo kasi nao ni OilCom nadhani wanaongoza
 
Bila kuwasahau oilcom tabata segerea ni nomaaaa, mi niliweka mafuta ya 20000 nkakiwasha kuelekea kinyerezi ile nafika magereza pale darajani taa ikawaka nlitukana njia nzima
pole sana mKuu. ulikuwa pekeako au na shemeji?
 
Victoria wengi wanapasifia
Sheli zake ziko maeneo yapi na napi mkuu
 
Puma (BP) ya Sinza Kijiweni ndio funika ya vituo vyote Tanzania kama sio East Africa,
Pale ukienda inabidi muda wote ukodoe macho kwenye Readings zao,
Otherwise kama kabla alipita tuseme bajaji akajaza labda Tshs 3,000/= nawe wataka ya Tshs 10,000/= basi zile za bajaji hazifutwi na zinajumlishiwa kwako hivyo ukilipa Tshs 10,000 unapata mafuta ya Tshs 7,000/= tu. Huu mchezo wanao pampu zote zilizoko pale Sinza Kijiweni kuna mimama pale ukiiangalia tu usoni unajua kabisa ni mipigaji.

Cha ajabu wanapenda kukwambia usogee mbele hata kama pale ulipo mpira unafika
 
Jibu swali wewe, wacha kuhororoja na kubwabwaja bila mpango:

Hivi vituo vya "shell" bado vipo?
Haya nakujibu,
"Shell" hawapo walikwishaondoka. Ila baada ya hapo vituo vilivyofuatia tukavibatiza kwa mafuta jina la "Sheli".
Halafu hivi kuhoroja ni nini??
 
Hapa tunaweza kuwa tunawaonea wakati mwingine juzi nilikua kituo kimoja cha mafuta akaja mdada akaweka mafuta ya sh.3000 sasa mtu kama huyu kwanini asifikiri amewekewa upepo?...chamsingi ukitaka kuamini kama niupepo au mafuta jaza full tank zikiingia 80lts wakati tank lako ni 60lts basi hapo tutakua nahaki ya kuwahukum
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…