Mnaongeleaje wizi wa mafuta sheli, yaani kujaza upepo?

Mnaongeleaje wizi wa mafuta sheli, yaani kujaza upepo?

-omba risiti.
-angalia mashine ya pump ya mafuta imesoma kiwango ulichotaka.
**wamiliki wa kampuni za mafuta hawatambui wizi huu unaofanywa na wafanyakazi**
 
Hii imeshanitokea mara mbili hapo Dodoma.. Mara ya kwanza nilikuwa natoka Mwanza kwenda Dar.. Kufika Dodoma nikajaziwa upepo.. Nilifika kwa shida sana Morogoro maana ilibidi nibanie mafuta na ilikuwa usiku.. Mara ya pili nilikuwa naenda Singida na nikajaziwa upepo Dodoma.. Mpaka nafika Singida saa saba ya usiku taa ya mafuta ilikuwa inawaka...
 
BP ni kampuni makini, wana pesa na reputation duniani kote. Kwa taarifa yako ni kuwa walishajiondoa kitambo kwenye retailing ya mafuta TZ baada ya kuona soko 'limeingiliwa' na mamlaka zilizokuwepo kuridhia.

Kwa taarifa yako BP waliuza biashara zake kwa Puma ili kupata pesa ya kulipia FINE kubwa waliopigwa na serikari ya marekani baada ya mabomba yao kupasuka na kuchafua bahari ya eneo la Gulf of Mexico. Na biashara walizo uza ni za nchi nyingi za kusini mwa Afrika, huku wakiiacha Afrika Kusini kama sijakosea.
 
Aisee sinza kijiweni kituo cha Puma yaani ni waizi sana nimejaza mafuta ya 30 elfu kwenye harrier yangu bado taa ya kuonesha mafuta hamna inawaka yaani nilibishana nao sana wakaniambia harrier inatank kubwa niliondoka ila roho iliniuma sana kesho yake nikaenda mlimani city sheli iliyoko kwenye kona pale sijui inaitwaje nikaweka ya 20 elfu tu mshale wa mafuta ukaenda zaidi ya robo tank. Ndipo nikaamini kituo cha puma sinza kijiweni ni waizi
 
siku moja nipo na kirikuu yangu yule dada ananiambia sogea mbele nikamwambia aweke mafuta ya elfu kumi akaminyaaa weee nikaona ameweka mafuta ya elfu nane! nikampa elfu kumi nikamwambia nirudishie chenji yangu elfu mbili akashtuka akasema eti ameweka ya elfu kumi nikamwambia mbona nimekushuhudia umeweka ya elfu nane? kwa aibu yake akaongeza mafuta ya elfu mbili! hapo ilikuwa Oilcom ya zamani pale kwa kopa! haya juzi nimeenda na suzuki van yangu mpaka puma ya mwanamboka baada ya hapo gari ikawa inabadilika mlio halafu haina nguvu kumpelekea fundi leo kafanya uchunguzi wake kumbe mafuta ni machafu na yamechakachuliwa na maji! Roho imeniuma sana itanibidi nirudie enzi zangu za kununua mafuta kwenye dumu la lita ishirini na walipokuwa wananiona na dumu langu kama hawajaniona vile wanahudumia magari kwanza mpaka boda boda lakin mwenye kidumu unawekwa nyuma na msonyo juu!
 
Kuna sehemu Doma, nilienda na bodaboda yangu nikatoa elf 5000, kwanini pikipiki isinizimikie njiani....nahisi niliwekewa mafuta ya 1000, elfu 4000 yote ilikuwa ni upepo.
 
Mmmh hichi kituo cha mafuta kinachoitwa shell kipo maeneo gani kwa dar
Hahaha! Mazoea tu hayo ya watanzania ila hakipo.Nadhani Shell walikuwa ndio wakwaza kuanza kuuza mafuta kwenye soko la retail, so watanzania wakajikuta wanazoea hilo jina na ikawa kawaida kwa watu kuita jina la kaampuni ya Shell kwa kila kituo.
 
Watanzania tuwe na tabia ya kudadisi au kutoa taarifa kwa taasisi husika pale inapotokea jambo ambalo si la kawaida.

KAMA sikosei taasisi inayohusika na masuala ya Vipimo ni WAKALA WA VIPIMO.

Ukiona unahisi umepunjwa mafuta toa taarifa ofisi ya Wakala wa Vipimo iliyopo karibu yako.

Ili kupunguza tatizo kama lipo toeni taarifa kwa wahusika. Kwa DSM ofisi zao zipo Jengo la NSSF Ilala Boma.
 
TSN Bamaga walishawai kunipiga baada ya mafuta ya elfu 20000 akaweka ya elfu 15000 ile nageuka kuangalia naona anabonyeza namba ili isome 20000 sikusogeza hata gari nikashuka na kumvaa yule mjaza mafuta akataka kuleta za kuleta nikamwambia sitoi gari mpaka aje meneja ilibidi awe mpole akaniongeza wese la buku 5 nikasepa
 
Hahaha! Mazoea tu hayo ya watanzania ila hakipo.Nadhani Shell walikuwa ndio wakwaza kuanza kuuza mafuta kwenye soko la retail, so watanzania wakajikuta wanazoea hilo jina na ikawa kawaida kwa watu kuita jina la kaampuni ya Shell kwa kila kituo.
Ok hapo sawa nimekuelewa asante
 
BP ni kampuni makini, wana pesa na reputation duniani kote. Kwa taarifa yako ni kuwa walishajiondoa kitambo kwenye retailing ya mafuta TZ baada ya kuona soko 'limeingiliwa' na mamlaka zilizokuwepo kuridhia.
hawajajipndoa Bali bp iliuzwa kwa puma energy! usitoe taarifa za uongo kama hauna data
 
Back
Top Bottom