Mnaonunua magari, kuweni makini na usanii huu msije kujuta

Mnaonunua magari, kuweni makini na usanii huu msije kujuta

MTV MBONGO

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2016
Posts
1,281
Reaction score
1,251
Kuna wimbi kubwa la usanii Wakati unapouziwa gari kwenye showroom: wateja wengi wanalalamika kuwa wauzaji wanaondoa Baadhi ya vifaa muhimu vya magari mf. Vifaa ndani ya Exhaust system n. k.

Kagua vizuri kabla na uende kununua ukiwa na fundi gari. Wengi hawakagui, wanastuka Baadae wanapopeleka magari service au yakianza KULETA Shida.

TUWE MAKINI.
 
Hao watu wa showrooms nao wawe na huruma. Gari ni used tena mnamuibia mteja.
Wale vijana pale show room ndio wanaagizwa hivyo vifaa/spare na washkaji then wanakwenda kuuza.
Ukitaka spare yoyote ukieaona wale wanaoaminiwa kuingia showroom utavipata ili isiwe side mirror au kioo Cha mbele.
Kuna watu wako tayari kuwauza mama zao kwa ajili ya pesa ya pombe
 
Yaani showroom wanaiba vifaa vya Gari wanalo muuzia mteja wao!!

Kuna vitu vinafanyika haviingii akilini kabisa, yaani mtu anaharibu sifa ya showroom yake kwa tamaa ya vitu vidogo vidogo?

Hizo showroom waweke CCTV camera na wezi wote wawatimue kazi ili wakajue life lilivyo kitaani coz wanawaharibia sifa na uaminifu toka kwa wateja wao.
 
Kuna wimbi kubwa la usanii Wakati unapouziwa gari kwenye showroom: wateja wengi wanalalamika kuwa wauzaji wanaondoa Baadhi ya vifaa muhimu vya magari mf. Vifaa ndani ya Exhaust system n. k.

Kagua vizuri kabla na uende kununua ukiwa na fundi gari. Wengi hawakagui, wanastuka Baadae wanapopeleka magari service au yakianza KULETA Shida.

TUWE MAKINI.
Wanatoa utumbo, inafanya gari isiwe na nguvu kabisa....

Sent from my SM-A505FN using JamiiForums mobile app
 
Yaani showroom wanaiba vifaa vya Gari wanalo muuzia mteja wao!!

Kuna vitu vinafanyika haviingii akilini kabisa,yaani mtu anaharibu sifa ya showroom yake kwa tamaa ya vitu vidogo vidogo?

Hizo showroom waweke CCTV camera,na wezi wote wawatimue kazi ili wakajue life lilivyo kitaani coz wanawaharibia sifa na uaminifu toka kwa wateja wao.

Cctv haiwezi saidia! Hizo gari zinachakachuliwa hata kabla hazijaingizwa huko show room!
 
Wanasema ukikagua gari show room na ukaridhika nayo chukua hapohapo. Kama utasema nakuja baadae au kesho na kweli ukaonesha nia ya kurudi, hapo ndipo uhuni hufanyika wa kubadirisha vitu.
 
Back
Top Bottom