Hawa watu sometimes sio kwamba wanapenda ni hali ya maisha...Kaka ukitaka kujua kuna wengine wanalia moyoni just kaa nao chini wafanye rafiki waulize watakwambia mengi sana na hapo ndo utaamini watu wanapitia maisha magumu.....
Kuna wakati mtu anakosa cha kushika na hajui afanye nini.
So bila kuwahukumu wafanye rafiki waulze wanataka nini,Na kwanini wako pale kama ni chakula wasaidie mnunulie hata kigunia cha mchele (kama una pesa) au mpe pesa kama ni kodi mlipie kodi naamini watabadilika...saa zingine muite piga naye stori muulize kwanini anafanya hivyo watakuambia..na kama ni shida tatua shida yake (Bila kuichakata mbususu) atakuheshimu kama ndugu yake.....
Inasikitisha sana. Kuna kipindi nilikuwa Arusha napiga mishe fulani. Nikaenda kupata chakula stand ndogo bar moja maarufu inaitwa Washington.
Ilikuwa ni mchana. Kuna dada mmoja akawa amesimama pembeni ya barabara akawa ananiangalia sana. Alisimama pale kama dakika 30 hivi.
Ni binti mzuri sana. Nikaamua kumuita maana kwa muda niliokaa hapo, kiburudisho kilikuwa kinahitajika.
Nikamkaribisha msosi, akanywa kinywaji lakini kuondoka akawa hataki. Nikamuaga akaangalia kwa huruma sana, akasema tuondoke wote. Nikamwambia nimemuita nimpe chakula tu, akasema anataka kuondoka na mimi, nikamwambia mimi nimefikia lodge, na yeye ni mwanamke hatuwezi kwenda huko bila makubaliano yoyote.
Akasema hakuna shida, chochote nitakachompa ataridhika.
Alikuwa akiongea hivyo anaona aibu sana na almost anatetemeka. Ili kujua kama kweli hana shida nikamuuliza kwao ni wapi, akataja. Akasema anaishi na mama yake(ambaye ni mgonjwa sana) na mtoto wake ambaye amemuacha kwa sababu mama ni mgonjwa.
Nikamwambia kama kweli mama ni mgonjwa twende tukamsalimie, then turudi. Akakubali kishingo upande. Tukachukua bajaji tukaondoka kuelekea nje ya mji. Kabla ya kufika akapiga simu jirani akamletea mtoto kama wa miaka minne hivi, tukaenda kwao ambapo nilimkuta mama yake anaumwa sana. Hawezi hata kujisogeza. Kodi anapokaa imeisha hawajalipa kama miezi mitatu hivi, wameshapigiwa kelele sana. Yaani wanashindwa kuwafukuza sababu ya namna ya kumtoa huyo mama ndani.
Akanitambukisha kwa mama yake eti mimi ni rafiki yake, amenipeleka nikamsalimie.
Kwa hali niliyoikuta pale, nilimpa 150K, ili anunue chakula na aweke mambo Sawa, nikamuahidi kesho yake tuonane ili tukamilishe jambo letu(namna ya kumtoka).
Nilipotoka pale ikawa ndio mwisho wa kumuona maana alipiga sana simu bila mimi kupokea (ni lazima nifanye hivyo kwa sisi wenye familia akizoea inaweza leta shida kwenye familia.)
Kuna watu wanafanya hii kitu sio kwa kupenda kabisa, mambo yanakuwa magumu sana upande wao(japo haifanyi wanachokifanya kuwa sahihi)