Mnaooa au kuolewa na wanaotegemewa katika familia zao changamoto mnazopitia kujenga maisha yenu

Mnaooa au kuolewa na wanaotegemewa katika familia zao changamoto mnazopitia kujenga maisha yenu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Yule aliyeinuka mmoja tu kwenye familia. Anategemewa na familia nzima na kuna wakati anasahau kuwa ana familia yake. Anawaza amalize nyumba ya wazee, ada ya wadogo zake, chakula chao cha kila siku.

Kwakua huyu ndiyo mtoto nyota wanaona hata wewe mume:mke unawazibia kwa mtoto wao. Pasi kufahamu ya kuwa mshahara wako unahudumia mambo mengi ya ndani.
 
hivi wewe mwanangu ukiolewa utaacha kuniletea mahitaji?

Sent using Jamii Forums mobile app
Unatakiwa uandae uzee wako, uache kuwa tegemezi kwa watoto. Maisha yenyewe haya, ukiwa tegemezi unawaumiza watoto.

Watoto wakuletee vile wakipata, lakini isiwe lazima kila mwezi ili wewe uishi angalau 60s, ukifikisha 75 huko ni sawa kuwategemea(kibongobongo)
 
sawa Eli79 ni wazo tu, wapo wanaotegemea watoto 100% na hivyo ndiyo walivyo. Utafanyaje?
Unatakiwa uandae uzee wako, uache kuwa tegemezi kwa watoto. Maisha yenyewe haya, ukiwa tegemezi unawaumiza watoto.

Watoto wakuletee vile wakipata, lakini isiwe lazima kila mwezi ili wewe uishi angalau 60s, ukifikisha 75 huko ni sawa kuwategemea(kibongobongo)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umasikini ni kitu kibaya zaidi kuliko hata kifo...
Hapo utakuta wazazi wanamtegemea mtoto wao ili walau aje aokowe familia yao (sio familia yake). Na hapo wanasahau kwamba kijana sasa ni wakati wake wa kutengeneza maisha yake pamoja na familia yake.
Haya yote ni sababu ya umasikini.
Wakati huo kijana nae anajikuta anasahau kufanya maisha yake na hata familia yake kwasababu tu anawaza ufukara wa wazazi wake.
Hii yote ni sababu ya umasikini.
Ninauchukia sana umasikini....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuwatunza wazazi ni lazima hata iweje.Chamsingi wewe ni kuangalia uwezo wako ili ubalance.Familia yako uihudumie na wazazi pia wapate huduma.Usiforce kuwajengea nyumba kama uwezo hauruhusu bali wapate huduma muhimu kama chakula mavazi malazi na matibabu.Huwezi kuacha wazazi wako wanalala njaa,wanatembea uchi wewe unahudumia MKE au Mme Na watoto tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom