Farolito
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 12,001
- 27,175
Wakuu,
Kumekuwa na tabia ya wamiliki wa magari hasa magari binafsi kutoa mabampa(bumpers) ya mbele au nyuma na kuweka ya chuma wakiamini kwamba ndio gari itakuwa imara na Salama zaidi kama itapata ajali ya kugongana uso kwa uso au wakati mwingine wanaweka Ngao ya Chuma mbele wakiamini gari itakuwa ngumu na Salama kama itagonga mti au kitu kigumu lakini wanajidanganya,iko hivi;
Katika ajali,gari isiyovunjika au kukatika itakuwa ni majanga kwa abiria waliopo ndani.
Magari ya zama hizi yametengenezwa kuvunjika na kukatika vipande mbele na nyuma ili kupunguza nguvu ya mgongano(impact) kwa abiria waliopo ndani.
Hivyo gari zimetengenezwa katika mfumo wa 'crumple zones'(maeneo ya kuvunjikia) na hizi zipo mbele na nyuma na inaanzia pale ambapo bumpers za plastic zinaanzia,kwa mbele inaanzia kwenye bumper mpaka inapoishia injini,na nyuma pia inaanzia kwenye bumper mpaka inapoishia buti ya mzigo.
Pia bodi ya gari za sasa zimeungwa kwa vipande vya vyuma ambavyo hivi inapotokea impact huvunjika au kuchomoka kwa nje ili kunyonya(crumple) ile nguvu ya mgongano tofauti na gari za zamani ambazo bodi lilikuwa linaungwa na chuma linalounganisha gari nzima.
Kwahio bumpers zimewekwa laini ili gari inapogongana zivunjike au kupasuka na kuruhusu ile force iendelee kubomoa hizi crumple zones na wakati huohuo katika kuharibiwa ndio inayonya na kupunguza force kumfikia abiria ndani,kifupi hizo Bampa ni kama godoro linamzuia mtu aliyeanguka kutoka juu ya bati ambapo godoro ndio litabeba ile force aliyonayo muangukaji na hivyo kuzuia madhara kwake.
Kwahio unapoweka bumper la chuma au Ngao ni kwamba unazuia mchakato huu kufanyika na hivyo ile force ya mgongano moja kwa moja itakufikia wewe na kukuua.
Hii iliwekwa ili kuzuia kinetic energy kwa namna salama(Energy is force by distance) kwa hio ukiongeza distance unapunguza force.
Kwahio kunapotokea mgongano zile crumple zones zitapokea ile impact ya ajali na kuisafirisha katika maelfu ya viajali vidogo vidogo ili kupunguza ile nguvu ya mgongano mkuu kukufikia wewe uliyeko ndani kwa wakati mmoja.
Kwahio kila kipande cha bumper kilichopasuka au kila bati linalopinda jua limenyofoa ile nguvu ya ajali iliyokuwa ikufikie wewe,tofauti na hapo ile force ingekukuta wewe kama ilivyo.
Kanuni ya Fizikia inasema kwamba kama unaendesha kwa spidi ya 50 mph na ajali ikasababisha gari isimame ghafla,abiria aliyeko ndani ataendelea kusafiri kwa spidi ileile ya 50 mph.
Sasa hapa utaona jinsi ambavyo kama umeweka machuma ambavyo ni magumu ile force itakubamiza mbele kwa spidi gani kama uko 100 Kph au 120 kph,hapo ndio ule msemo wa utumbo kuchanganyika na maini utapokamilika au ubongo kupasuka kama ulifunga mkanda,na kama hukufunguka mkanda fikiria utaenda kutupwa kilomita ngapi kupitia kioo cha mbele kabla ya kufa.
Kwahio nashauri haya marekebisho ya kuweka chuma mbele muache,waliotengeza gari walipima ni namna gani gari itaumia ili kukulinda wewe uliyeko ndani ila wewe unataka uilinde gari isiumie bila kujali usalama wako.
Kama huamini fuatilia ajali za magari ya STK,STL nk, hasa za uso kwa uso uone ni wangapi huwa wanatoka salama,nyingi zimewekwa vyuma mbele.
Picha za maelezo zimeambatanishwa.
Asante.