Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,168
- 39,118
Imekuwa kawaida Sasa Mh Rais au viongozi wa chini yake wanapotoa kauli tatanishi, za kukera au zilizo kinyume na sheria au hata katiba ya Nchi, huwa kunajitokeza wapambe kufafanua na kusema Rais kanukuliwa vibaya utadhani wao ndo wana hatimiliki ya uelewa.
Pia soma Rais Samia: Mnaotudai fidia kuweni na subira tumalize miradi ya maendeleo kwanza ndipo tuwalipe
Sijawahi kuona Ikulu ikiomba radhi Kwa kauli za kupotoka au zinazoumiza watu. Ni juzi nilishangaa kuona TRC wanaomba radhi kwa hitilafu ya SGR lakini nao wakaja na drama (maana halisi ya drama) kwamba sababu ya hitilafu ni michezo ya Mr Bundi na Bw. Ngedere wanaochezea nyaya za umeme.
Mh Rais akiwa Morogoro baada ya kupokea Malalamiko ya Wananchi waliovunjiwa nyumba na kuharibiwa mashamba kupisha miradi ya serikali ikiwemo SGR alitoa kauli kwamba serikali itafanya maendeleo hata Kwa kuvunja Mali za Wananchi ili kuharakisha maendeleo lakini baadaye itawafidia Wananchi Kwa vile hela za miradi ni za kudunduliza.
Kauli hii imezua Malalamiko toka Kwa waliovunjiwa, wanasiasa pinzani, wanasheria na wanaharakati wakieleza kuwa ni uonevu Kwa Wananchi masikini wanaojibana kujijengea makazi yao lakini baadaye wanavunjiwa makazi wanarudi kuwa wapangaji wakisubiri kulipwa fidia ambayo hawajui watalipwa lini.
Kiujumla ni mateso Mtu mwenye makazi kukosa makazi ghafla tena Kwa sababu ya janga la makusudi ambalo linaandaliwa Kwa Muda mrefu na inajulikana ujenzi wa barabara au reli ni mipango ya Muda mrefu Kwa nini fidia isiwe kipaumbele kama Ibara ya 24 ya Katiba ya Tanzania inavyotaka?
Lakini safari hii tofauti na wakati mwingine Vijana wanaomiliki uelewa wa Watanzania Kwa kufafanua kauli za viongozi na kusema wamenukuliwa vibaya wamechelewa Sana kutuletea ufafanuzi wa kauli hii inayoonyesha ukandamizaji wa Serikali Kwa Wananchi wake.
Hebu waje watufafanulie Sisi Wenye akili nzito tusije tukaingia kwenye mtego wa wapotoshaji.