Mnaosema kuwa Mo hajaweka bilioni 20 Simba, hizo Bilioni 20 za kitu Gani?

Hivi huyu MO anawapa shilingi ngapi ili muandike postings za kipuuzi kama hizi? Mwanzoni aliwapa pesa kupost kumtukana Mangungu sasa kaona haikulipa mnaanza kupost kumsifu na kumtetea dhidi ya lawama anazoshtumiwa. Huu umaskini duuuuuu
Kwanza Mimi Sina mahusiano na Mo. Mimi ni mshamba wa Kigungawe Iringa.

Humu Kuna mada inaitwa "ukweli kuhusu uwekezaji Wa Mo Dewji Simba ndiyo huu"

Hiyo mada kaisome nimeandika Mimi.

Hili ni jambo jingine kabisa.

Wengine hatujawahi kuwa na "Price Tag" maishani mwetu.
 
Asipoelewa na hapa usimjibu tena.
 
Mleta mada acha upofu.
Kwani mapato ya Simba na pesa za CAF huwa nani anachukua au zinakwenda wapi?
Pesa za wadhamini nani anachukua?

Mo pale Simba ni mwizi tu, hana chochote anachotoa na hana chochote anapoteza, yuko pale kuvuna. Mpaka sasa hajatoa hata senti tano na ana kiri wazi kuwa hawezi kutoa pesa ya uwekezaji mpaka mipango ya ndani ya kisheria iwe tayari.
 
Na kumnunua Ayubu 3b Tshs.
 
Huo mnaouita uwekezaji wa Mo simba wa billioni 20, atakuwa anamiliki hisa kiasi gani ya hiyo club?

Kwa upande wa Yanga, sijasikia hata siku moja huyo business partner wa mkwere GSM kuwa amewekeza Yanga!! GSM ni mfadhiri/shabiki wa Yanga.
 
Nia ya mo kuwekeza ni kuibadilisha Simba iendeshwe kisasa na sio kutegemea mapato ya mlangoni. Kitendo cha Simba kumtegemea mo kinaondoa maana nzima ya uwekezaji kwani Simba ilishapitia vipindi tofauti vya wadhamini akiwemo mo mwenyewe.
Mo kabla ya kuingia uwekezaji alisema anataka Simba iwe level ya mazembe au Al ahly lakini he tumeshafikia level zao Kama kununua wachezaji wa Bei kubwa, kumiliki uwanja na kuzuia wachezaji wetu Bora wasiuzwe.
Kabla ya kuingia alilaumu Simba kuuza wachezaji wao wazuri lakini tangia aingie Simba imeuza wachezaji wengi wazuri Tena wanaficha hata Bei.
Simba mpaka Sasa haijaonyesha mpango wowote wa kujenga uwanja ukiacha mpango wa kuchangisha wapenzi na mpaka Sasa hakuna taarifa ya pesa zilizochangwa.
Amezuia wawekeza Kama Bakhresa waliotaka kuwekeza Simba kwa miaka 10 kwa kisingizio brand ya Simba ni kubwa kuliko yanga na Simba wakiishiwa atatoa pesa mfukoni kwa lugha nyingine hataki Simba jitegemee.
Tumeshindwa kushindana kusajili wachezaji wazuri kwa sababu ya kushindwa kwa nguvu ya pesa
 
Dah! Mnahuzunisha sana kwa kweli! Kwani yale mabilioni ya hela mnazopata kutoka kwa wadhamini wenu mfano NBC, Azam Media, Mbet, Mo xtra, Mo foundation, Mo janja janja, nk; huwa mnafanyia nini? Mpaka mumtegemee mtu kwa kila kitu?

Na hapa sijataja zile hela mnazopewa na CAF kwa kushiriki mashindandano ya Kimataifa!! Ada na michango mbalimbali kutoka kwa wanachama!! Hela za viingilio, mauzo ya jezi, nk.
Na kwa nini mna mfumo mbovu hivi wa kuendesha timu yenu? Yaani Mo peke yake ndiye anayelipa mishahara ya wachezaji, anasafirisha timu ndani na nje ya nchi, nk!! Aisee kama ni hivho, basi kazi anayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…