Baada ya mfalme Suleiman kufa watoto zake wawili Rehoboam na Yeroboam walianza kugombania utawala. Lakini Yeroboam alikua kashapewa unabii kwamba Ufalme wa waisrael utagawanyika.
Sasa basi Rehoboam alipewa atawale makabila mawili ya Yuda na Benjamin wao walikaa huko Yerusalem. Neno wayahudi limetokana na jina Yuda yaani watoto wa Yuda.
Yeroboam alitawala makabila kumi yaliyobaki.. Hivo basi Kila myahudi ni muisrael kwakua antoka chimbuko la Baba yao Israel/Jacob ila sio kila muisrael ni myahudi/mwana wa yuda. Maana makabila yalikuepo 12.
Sijui nimeeleweka....
Unabii wenyewe huu hapa!
1 Wafalme 11:29-31
[29]Ikawa zamani zile Yeroboamu alipokuwa akitoka katika Yerusalemu, nabii Ahiya, Mshiloni, alikutana naye njiani; naye Ahiya amevaa vazi jipya, na hao wawili walikuwa peke yao mashambani.
[30]Ahiya akalishika lile vazi jipya alilokuwa amelivaa, akalirarua vipande kumi na viwili.
[31]Akamwambia Yeroboamu, Twaa wewe vipande kumi, maana BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nitaurarua ufalme, na kuuondoa katika mkono wa Sulemani, nami nitakupa wewe kabila kumi,