Mnaotaka kufanya kazi na wanaojiita Nickshine Media Production kuweni makini sana

Haina neno, tutajadili tuafikiane, shukrani sana kwa kunijibu vizuri
Tunaoffer packages za aina nne.

Kuna Basic, Ordinary, Advanced na Executive the lowest being Basic package and the highest ni Executibe package.

Basic Package inajumuisha:
  • Coverage ya event nzima kwa picha na video.
  • Projector 2 kwa ajili ya live shooting.
  • Albamu itakayokua na picha 160 size ya 5/7.
  • Nakala tatu za DVD.
  • Flash itakayokua na picha na video za tukio.

Kulingana na package kuna vitu vitaongezeka au vitabadilika ila ambacho hakitabadilika ni ubora wa picha na video zako na delivery ya kazi kwa mteja. Two weeks baada ya event tunakukabidhi mzigo wako.
 
Shughuli ni simple, sitahitaji hizo projector, halafu ukitegemea upo dar, nauli kwangu,, naona hatutawezana ila umejitangaza wadau wanakusoma naamini utapata wateja,, kila la heri
 
Wengi nadhani ni shule ndogo na hawana exposure Mimi Kuna wapiga picha was chugga huwatafta na huwa nagharamia wako humble kazi zao nzuri huwa wanaendaga kupiga picha Hadi Nairobi na hawana longolongo hao vijana ila Hawa was Dar hamna kitu
Siyo wote una bahati mbaya umekutana na watu miyeyusho ila kama umewahi kusikia sehemu inaitwa Get Real Training ndipo timu yetu ilikutana tukiwa tunafanya mafunzo ya video production, shooting etc.

Baadhi walienda kwenye tamthilia maarufu ya Siri ya Mtungi na wengine tukasogea kwenye deals za kufanya still picture na shooting. So tunajua tunachofanya.
 
Shughuli ni simple, sitahitaji hizo projector, halafu ukitegemea upo dar, nauli kwangu,, naona hatutawezana ila umejitangaza wadau wanakusoma naamini utapata wateja,, kila la heri
Yea kweli kama ni hivyo itakupa unnecessary costs.
 
Eti ngumbaru[emoji1787]
 
Hizi Screenshots tunaweza kuprove kwamba ulikuwa unatuma kwa Nicki? Hata kublue Tick haijatick, namba ya Nicki akisoma inablue Tick.

Dada acha kua na spidi zisizo na maana, mimi tangu nachangia huu uzi nmesema kabisa vendor wangu hakua Nick, vendor aliyefanya kazi namimi hata akipitia huu uzi na kuona hizi screenshot ataelewa kuwa ni yeye maana kwangu na kwake kwenye simu zipo!! Na mimi sijataka kumtaja jina kwa sababu hata baada ya kutufanyia ubaya sikua na nia ya kuja kumleta huku kwenye mtandao na huu uzi haujaanzisha kwa ajili yangu, mimi nimechangia kutokana na kilichonikuta.
Alafu pia acha ushamba, namba ikisoma ina blue tick nini?? Mimi nmemute read recepients ingeblue tick kivipi? Kama hujui uliza.
 
Inawezekana huyo mtumaji ndiye mhusika ila anakuja kujifanya naye ni mhanga.

Mitandao hii ni balaa

Mimi sina haja ya kujieleza zaidi ya hapa ila naamini aliyefanya kazi ya shughuli yangu ya harusi akipita hapa ataelewa na naamini pia atabadilika for good. ( narudia tena kwa upande wangu mimi vendor hakua Nickshine).
 
Sina hamu na washona suti vijana wa kibongo, nikipata event yoyote bora ninunue nguo kuliko kwenda shona suti.

Mshona suti ambaye anaustaarabu angalau kwa upande wnagu naona ni Jm na Mtani kwakweli, wanazingatia muda wa kumaliza kazi ya mtu na hata kama pana excuse wanakujulisha, sitaki kukumbuka nilimsindikiza ndg yangu na kwa suti bega kushona suti ya shughuli yake yaliyotukuta tulikoma ni ahadi za njoo kesho njoo keshokutwa ikisindikizwa na kubadilishiwa aina ya kitambaa alichochagua na uzuri alipiga picha wakati anachagua[emoji3525][emoji847] .
 
Najiuliza iweje wewe ushindwe kumpata hewaaani huyo Nick ila rafiki yako ampate. Nick tulia.
 

Washona suti wengi janja janja, wanapeleka kazi zao kwa mafundi ambao pia wanafanya kazi za kimtaa
 
Mimi sina haja ya kujieleza zaidi ya hapa ila naamini aliyefanya kazi ya shughuli yangu ya harusi akipita hapa ataelewa na naamini pia atabadilika for good. ( narudia tena kwa upande wangu mimi vendor hakua Nickshine).
Code za lugha yako inakukamatisha vizuri.

Endelea kufunguka
 
Mkuu kwani unakimbizwa au unadhani kila mtu anawajua hao watesi wako, unapoleta habari ungetuambiwa wako wapi,ni kipi uliharibiwa na makubaliano yenu yalikuwaje? hii story imekuwa nyepesi sana haina uzito na mwisho tutaona kama ni vita vya kibiashara tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…