Mnaotamani kuja Dar es salaam hii ndio dar yenyewe je! Mtaiweza?

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
4,095
Reaction score
13,016
Ndugu zetu wa Mikoani hii ndio dar es salaam sasa, huku usafiri wa umma hasa nyakati za asubuhi na jioni bila kuwa mbabe haupandi.

Nimewahi kushuhudia dada mmjoa akiwa katika purukushani za kuingia kwenye usafiri ile vuta ni kuvute, akajikuta maziwa yote yapo wazi, na yeye hakujali wala nini akaendelea kung’ang’ana mpaka akaingia na siti akapata. Hii dar es salaam karibuni sana.


 
Hakuna kitu sipendi km usafiri wa mwendokasi.
Nilinusurika kubanwa na mlango, hadi Sandals yangu ilibaki nje, nilisafiri na sandals 1,
Sijawahi rudia na sipandi tena, km bajaji na boda nimekosa, bas ntapanda dala dala.

Mwendokasi hapana πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
 
Pole sana,
Kwahiyo ile Sandal moja uliitupa au umeiweka kama Kumbukumbu?
 
Dah!Kumbe wa Daslamu mmeanza kutumia ndege zisizo na siti tayari?Jipongezeni kwa kula miguu ya kuku na utumbo wake kufurahia hayo maendeleo yenu.Kudaadekii!
 
Mimi mkanda ulikatika aseeh πŸ˜‚
 
Hapo kuna watu wana-faint kila siku, acha kabisa huo usafiri, ni kero na ishara kubwa ya umasikini wa akili mkuu.
Usafiri wa kawaida tu ila kuna namna serikali inafeli , pia kama mtu hana ramani yakufanya huko daslamu bora abaki kijijini achunge mbuzi tu, kuliko kujaza ushuzi kwenye huo usafiri wa uma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…