Mbowe kafanya makubwa sana. Anastahili heshima na pongezi kwa aliyoyafanya.
Lakini wana- CHADEMA mnatakiwa kutambua kuwa binadamu anaweza kufaa sana kwa mazingira fulani kwa kazi fulani kwa wakati fulani lakini siyo lazima afae wakati wote kwa mazingira yote. Na siyo sahihi kwa sababu kiongozi alifanya vizuri sana wakati fulani aendelee wakati wote hata kwenye mazingira na nyakati asizozimudu kama shukrani kwa mazuri aliyoyafanya.
Ni kama CCM, ilitufaa wakati fulani kwa kazi fulani za wakati huo lakini kwa mazingira ya sasa haitufai tena. Ndiyo maana unakuta watu kama akina Kabudi, hata wakipewa nafasi ya kuongea, wanakazania kuongelea historia tu. Ni kwa sababu walionekana ni wasomi wazuri nyakati hizo lakini kwa nyakati hizi, wakiongea wanaonekana ni watu wasiojua kitu na waliopitwa na Ulimwengu uliopo.
Kwa mazingira ya sasa na kwa wakati huu, kwa kuyatazama mazingira ya siasa ya sasa, na hali ya CCM kwa sasa na uongozi wa CCM na serikali uliopo sasa, tunahitaji sana mbinu mpya, mtazamo mpya, fikra mpya na pengine viongozi wapya wenye ujasiri mpya.
CCM haitufai tena kwa mazingira ya sasa lakini kuiondoa kunahitajika mipangilio mipya kabisa. Siyo ile ya kale.