Mnaoteuliwa kumbukeni kulipa Imani na Amani

Mnaoteuliwa kumbukeni kulipa Imani na Amani

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Bila shaka aliyekuteua anafahamu machache sana kuhusu wewe ila mengi unayo wewe mwenyewe kwenye akili na moyo wako. LAKINI bila shaka aliyekuteua katanguliza IMANI kwako kuwa utaweza kumsadia yeye kwenye malengo yake. Hivyo Imani lazima izae Imani.

Wakati huohuo lazima ufahamu kuwa uteuzi wako na hata wa aliyekuteua sio wa kudumu milele, iko siku aliyekuteua na uliyeteuliwa mtaondoka kwenye nafasi zenu na kurudi uraiani, Hivyo kumbukeni kuna maisha baada ya kuondoka kwenye nafasi hizo.

Kama mkilifahamu hili basi wapelekeeni AMANI mnaowatumikia. Na Amani ni tunda la HAKI, nendeni mkaihubiri na kutenda kwa HAKI muda wenu wote. Kumbukeni kuwa haki na umaskini havikai chumba kimoja. Kaondoeni umaskini wa wananchi kwa akili na juhudi zenu zote.

Peke yenu hamtaweza bila kushirikisha watu vertically na horizontally, down top badala ya top down decisions.

Kama utashindwa kabisa kuacha alama njema kwenye eneo lako, basi usishindwe japo kupanda mti mmoja wa kivuli ili watu wakukumbuke nao wakati wakinywa kahawa chini ya kivuli chake.

Cheo ni dhamana, kamtangulizenu Mungu.
 
Back
Top Bottom