braza juzi nilijiunga kifurushi cha GB 7 cha mwezi na laini yao huwa naweka tu pale napotaka kutumia mb.kituko kilikuja kabla sijatoa laini huwa naangalia kiasi cha Mb zilizobaki,nlikuwa na GB 6.5 zilizobaki na ushahidi wa msg ninao wa salio,sasa nikatoa line jana naweka line nikataka kudownload kitu cha Mb30 mida ya saa tano asubuhi,
sms ikaja eti huna salio la kutosha nlipanic hatari ikabidi niwapigie huduma kwa wateja...daah YAANI NIKAAMBIWA UMETUMIA GB nyingi MIDA YA SAA 4 ASUBUHI WAKATI LINE NIMEIWEKA SAA TANO ASUBUHI?
Daah nlichoka nikawaambia hebu angalia hii line imkuwa hewani muda gani toka sasa?akabaki anacheka tu na kuniambia ndugu ndio hivyo umetumia mb nyingi muda huo...
Ila kitendo cha kucheka tu nikawa nimeshapata jibu kinachoendelea TTCL...
TTCL MNAZINGUA SANA YAANI HAMNA MTU ATAKAE KUBALI HUU UJINGA WENU