Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 790
- 1,316
Kuna mtindo umezuka sasa hivi, kila kona unapogeukia, kila mtu unayekutana naye anakwambia anza biashara ufanikiwe.
Mbaya zaidi ni kuwa maneno haya yanaambatana na kejeli haswa kwa watu ambao wameajiriwa kuwa ni duni na kwamba hawawezi kupata mafanikio.
Hii movement pamoja na kuwa na mazuri mengi, lakini inazo changamoto nyingi tu zinazohitaji tafakari ya kina.
Mosi, sisi watu hatufanani. Kuna mwingine anaweza nunua bizaa elfu 30 na akamuuzia mteja kwa laki na ishirini huku akilalamika hakuna faida kuficha ukweli.
Wakati kwa mtu mwingine kufanya jambo hilo kunamnyima raha na anajihisi kama vile anamuibia mteja wake.
Kimsingi, kufanya biashara ni kipaji kinachoambatana na roho ngumu sana. Kama hujabarikiwa kuwa na roho ngumu, sio rahisi kutoboa kwenye biashara.
Katika kuishi kwangu nimeshuhudua watumishi kadhaa, wamechukua mikopo, wakaanzisha biashara, ambazo zimeishia kufa na mitaji imepote.
Pili ni ecosystem ya maisha ya wanadamu. Ili maisha yaendelee, haina budi wawepo wanaouza na wanaonunua. Uwiano huu usipokuwa sawa, hakuna biashara itafanikiwa.
Jaribu kuwaza, hivi kila mtu akiwa dereva bodaboda, hii biashara ya bodaboda itawezekana kweli?
Tunahitaji tuwe na wafanyabiashara kariakoo, tuwe na madaktari muhimbili, tuwe na maprofesa UDSM, tuwe na wakandarasi, askari n.k
Tatu ni dhana potofu kuhusu maana ya mafanikio. Hela ni muhimu sana, ila sio kipimo pekee cha mafanikio. Sasa hivi ni kama neno mafanikio maana yake wewe ni wangapi katika orodha ya matajiri?
Kuna msemo wa kiingereza kuwa You can't judge a fish by ability to climb tree. Maana yake mafanikio yapimwe kwa eneo husika.
Kwa mfano, Samia sio mfanyabiashara mashuhuri, lakini kwenye eneo lake la siasa amefanikiwa. Nsekela na Vunja bei wote ni vijana au Samata na Diamond, utasema nani amefanikiwa na nani amefanikiwa?
Wapo watu dunia nzima inawajua kwasababu ya utumishi wao, mfano mzuri ukiwa ni Dr. Benn Carson. Na wengine wanajulikana kwa utajiri wao.
Maana yangu ni hii, mtu asikuvuruge kwa kukwambia fanya biashara wakati unajijua hata hiyo biashara huwezi. Fuata wito wako wa ndani! Maadamu unamudu maisha yako vizuri, jiongezee thamani na kujituma, hapo hapo ulipo mafanikio yako yatakuja.