Mnasema tufanye biashara, kazi tunazofanya afanye nani?

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
790
Reaction score
1,316
Kuna mtindo umezuka sasa hivi, kila kona unapogeukia, kila mtu unayekutana naye anakwambia anza biashara ufanikiwe.

Mbaya zaidi ni kuwa maneno haya yanaambatana na kejeli haswa kwa watu ambao wameajiriwa kuwa ni duni na kwamba hawawezi kupata mafanikio.

Hii movement pamoja na kuwa na mazuri mengi, lakini inazo changamoto nyingi tu zinazohitaji tafakari ya kina.

Mosi, sisi watu hatufanani. Kuna mwingine anaweza nunua bizaa elfu 30 na akamuuzia mteja kwa laki na ishirini huku akilalamika hakuna faida kuficha ukweli.

Wakati kwa mtu mwingine kufanya jambo hilo kunamnyima raha na anajihisi kama vile anamuibia mteja wake.

Kimsingi, kufanya biashara ni kipaji kinachoambatana na roho ngumu sana. Kama hujabarikiwa kuwa na roho ngumu, sio rahisi kutoboa kwenye biashara.

Katika kuishi kwangu nimeshuhudua watumishi kadhaa, wamechukua mikopo, wakaanzisha biashara, ambazo zimeishia kufa na mitaji imepote.

Pili ni ecosystem ya maisha ya wanadamu. Ili maisha yaendelee, haina budi wawepo wanaouza na wanaonunua. Uwiano huu usipokuwa sawa, hakuna biashara itafanikiwa.

Jaribu kuwaza, hivi kila mtu akiwa dereva bodaboda, hii biashara ya bodaboda itawezekana kweli?

Tunahitaji tuwe na wafanyabiashara kariakoo, tuwe na madaktari muhimbili, tuwe na maprofesa UDSM, tuwe na wakandarasi, askari n.k

Tatu ni dhana potofu kuhusu maana ya mafanikio. Hela ni muhimu sana, ila sio kipimo pekee cha mafanikio. Sasa hivi ni kama neno mafanikio maana yake wewe ni wangapi katika orodha ya matajiri?

Kuna msemo wa kiingereza kuwa You can't judge a fish by ability to climb tree. Maana yake mafanikio yapimwe kwa eneo husika.

Kwa mfano, Samia sio mfanyabiashara mashuhuri, lakini kwenye eneo lake la siasa amefanikiwa. Nsekela na Vunja bei wote ni vijana au Samata na Diamond, utasema nani amefanikiwa na nani amefanikiwa?

Wapo watu dunia nzima inawajua kwasababu ya utumishi wao, mfano mzuri ukiwa ni Dr. Benn Carson. Na wengine wanajulikana kwa utajiri wao.

Maana yangu ni hii, mtu asikuvuruge kwa kukwambia fanya biashara wakati unajijua hata hiyo biashara huwezi. Fuata wito wako wa ndani! Maadamu unamudu maisha yako vizuri, jiongezee thamani na kujituma, hapo hapo ulipo mafanikio yako yatakuja.
 
We kuna kitu hujaeleqa kabisa unahisi biashara ni kuwa Vunjabei tu kuuza nguo. Kile unachokifanya au ulichosomea una uwezo wa kukifanya kuwa interms ya biashara. Kivipi??

We ni daktari kusanya pesa yako ndani ya miaka 20 , nenda mbeya kafungue hospital yako kaa utulie itaingiza hela kuliko hio ajira yako , kesho na kesho kutwa watoto watarithi jina na hio hopstal hata wakisoma wanajua baba ana hospital tutasmamia

Mfano mwngine : We ni Engineer wa magari unakubali kuajiriwa ili kupata mtaji then baadae unafungua garage yako unapiga kazi

Punguza uoga wa biashara , Ajira ni utumwa , kataa kuajiriwa. China na waarabu wanapiga hatua sana kwasbb hizo hawaajiriwi hovyo hovyo

Sasa usije kuniuliza je ukiwa pilot nd ununue ndege zako ntaona akili zako fupi sana πŸ˜„ kuwa kwanza pilot nd uje nkushaur
 
Akili za kuambiwa changanya na zako. Ili uweze kuishi ni sharti uwe na namna flani yyt ile ya kukupa kipato.

Maisha hayana formula maalumu
 
Kingine ni kuwa hauhitaji jamii ya watu ndio ikuthibitishe mafanikio yako. Kufanikiwa kwa mtu ni jinsi wewe unavyochukulia, hizo zingine ni kelele za chura tu
 
Kingine ni kuwa hauhitaji jamii ya watu ndio ikuthibitishe mafanikio yako. Kufanikiwa kwa mtu ni jinsi wewe unavyochukulia, hizo zingine ni kelele za chura tu
Hili nalo ni bonge la neno! Ahsante sana comrade
 
Comrade hoja yangu ni kuwa biashara ni kipaji, ambacho kama huna huna tu!
Inawezekana biashara zimewatoa wengi, lakini tukumbuke pia zimewaumiza wengi.
Sio kila mtu anaweza kufanya biashara akafanikiwa.
 
Na sio kila mtu kwa asili ni mfanyabiashara. Uwezo wa kubembeleza mtu anunue sina, unanilazimisha nifanye biashara. Wawaache watu wafanye kinachowavutia.
 
Kaa sebuleni angalia TV.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Comrade hoja yangu ni kuwa biashara ni kipaji, ambacho kama huna huna tu!
Inawezekana biashara zimewatoa wengi, lakini tukumbuke pia zimewaumiza wengi.
Sio kila mtu anaweza kufanya biashara akafanikiwa.
Biashara ni kazi tu kama kazi zingine na pia ni kazi inayojitaji hesabu na mambo mngn tu kidg ya kuzingatia , ukisema kipaji unakosea.

Zingatia ununuaji na uuzaji na unachokipata uki invest kwenye hio hio biashara au nje basi inatosha. Ni mbinu tu ndogo
 
Na sio kila mtu kwa asili ni mfanyabiashara. Uwezo wa kubembeleza mtu anunue sina, unanilazimisha nifanye biashara. Wawaache watu wafanye kinachowavutia.
Nani kasema kila biashara ni kubembelezana , ukiona unabembeleza mtu kweny biashara yako bas hio biashara kuna mahal umekosea either bei au quality

Biashara ni ushawishi namna gan utamshawishi mtu anunue unachokiuza zingatia huduma zako na quality hivo tu
 
Sio kila mtu pia ana uwezo wa kushawishi watu. It doesn't matter what words were used, iwe kubembeleza au kushawishi, thats not the point. Swala ni uwezo wa mtu sio neno lililotumika
 
Achana nao hao wanaokuambia ufanye biashara wewe ishi tu usijifananishe na mtu ushawai kuona nzi anajifananisha na nyuki? usizidiwe akili na nyuki.
 
Na sio kila mtu kwa asili ni mfanyabiashara. Uwezo wa kubembeleza mtu anunue sina, unanilazimisha nifanye biashara. Wawaache watu wafanye kinachowavutia.
Unambembeleza mteja ili iweje? wewe kaa kwenye biashara yako endelea kuchati hakikisha umejikamilisha mteja atakuja mwenyewe. Biashara ni lazima kazi za kuajiriwa Zina kikomo.
 
Sasa na nyie mbona mnasema tufanye kazi wakati hizo kazi mnafanya wenyewe πŸ˜ƒ πŸ˜ƒ πŸ˜ƒ πŸ˜ƒ πŸ˜ƒ πŸ˜ƒ πŸ˜ƒ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…