Uchaguzi 2020 Mnataka tuendelee kuwa na Rais wa miundombinu? Ingekuwa miundombinu ndiyo kipaumbele cha mtu wachina wasingekamatwa kwenye makontena wakizamia Ulaya

Duniani kote wanaharakati na wapigania haki za binadamu huwa wanafadhiliwa ivyo hakuna mtu atakaye kuwa tayari akupe ufadhili bila kuwa na agenda nyuma yake,wanaharakati na mawakili hawawezi kuendesha nchi.
 
Huyu mgombea ambaye ndiye Rais amalizaye muda wake na anaomba tena watanzania wampe tena miaka mingine 5 ili aendeleze kipaumbele chake kwenye kununua ndege, kujenga madaraja, kujenga reli, kujenga viwanja vya ndege na yanayofanana na hayo.

Lakini hebu tujiulize ameyafanya hayo miaka yote 5, Je! Mtanzania wa kawaida anayependa kumuita mnyonge amenufaika na nini? zaidi ya kushuhudia ugumu wa maisha kila kukicha?

Rais ambaye unapotaja maendeleo yeye akilini mwake huja flyover, madaraja, reli na midege huyu hatufai.

Rais amabye unapotaja kuboresha afya yeye akilini mwake huja majengo anayoyaita hospitali bila kuangalia soft elements ambazo ndiyo muhimu mfano idadi ya madaktari wanaolipwa vizuri, madawa na vifaa vya matibabu.

Nawakumbusha watanzania kuwa kwa sasa hakuna nchi yenye miundombinu ya kustaajabisha mfano wa flyovers, madaraja, reli duniani kama China lakini raia wake kila kukicha wanazamia kuja Ulaya, kila siku wanakamatwa kwenye makontena. Ukiwauliza tatizo nini ukiwa unafahamu kuwa China ni nchi tajiri kimiundombinu, watakwambia wanahitaji maisha bora na uhuru.

Sasa huyu kila siku yeye anasema anataka kuifanya Tanzania iwe kama Ulaya sijui anajua China iko Ulaya? ni bora angekuwa anasema anataka kuifanya Tanzania kuwa kama China (kitu amabacho nacho hawezi) tungekubaliana naye lakini kwa ubora wa maisha amekwishafeli.

NI WAKATI SASA WANANCHI KUCHAGUA IKIWA MNATAKA RAIS AMBAYE ATAJENGA MIUNDOMBINU AKIBORESHA MAISHA YENU PIA, AU RAIS AMBAYE KWAKE YEYE MAENDELEO NI MIUNDOMBINU PEKEE BILA KUBORESHA MAISHA HALISI YA MWANANCHI NA KUMPATIA UHURU WAKE.

Ni wakati wa kuchagua Tundu Lissu ili ujengewe miundombinu huku maisha yako na uhuru vikiboreshwa ama John Magufuli ambaye tafsiri ya maendeleo kwake yeye ni ujenzi pekee huku akiminya haki za binadamu na kufuta uhuru wa kujieleza.

Jioni njema
Andiko zuri kabisa
 
Jitu linajifanya kushabikia sijui ndege sijui maendeleo ya madaraja wakati ndege hajawahi panda na wala hana gari la kupitisha katika hilo daraja.
Harafu yeye choka mbaya mnyonge anajiita
kila aliyefanikiwa anamuona mwizi na freemason.
kama mkichagua tena mkapimwe akili maana mtakuwa mnamatatizo.
Wewe ulishawahi kuonja uhuru wa u guy huo mnaoutaka?
 
Bila wao watawala wa kiafrica wangekuwa wanatubanika live Kama nyama,waafrika hawana uwezo wa kujiongoza Ni lzm wauwane,waibiane,wawaumize wenzao,waibe kodi za wananchi,wapendelee kwao

kabla ya mzungu afrika kulikua na tawala zao ambazo hakukua na haya mambo uloyataja hapa.
 
Huyu mgombea ambaye ndiye Rais amalizaye muda wake na anaomba tena watanzania wampe tena miaka mingine 5 ili aendeleze kipaumbele chake kwenye kununua ndege, kujenga madaraja, kujenga reli, kujenga viwanja vya ndege na yanayofanana na hayo.

Lakini hebu tujiulize ameyafanya hayo miaka yote 5, Je! Mtanzania wa kawaida anayependa kumuita mnyonge amenufaika na nini? zaidi ya kushuhudia ugumu wa maisha kila kukicha?

Rais ambaye unapotaja maendeleo yeye akilini mwake huja flyover, madaraja, reli na midege huyu hatufai.

Rais amabye unapotaja kuboresha afya yeye akilini mwake huja majengo anayoyaita hospitali bila kuangalia soft elements ambazo ndiyo muhimu mfano idadi ya madaktari wanaolipwa vizuri, madawa na vifaa vya matibabu.

Nawakumbusha watanzania kuwa kwa sasa hakuna nchi yenye miundombinu ya kustaajabisha mfano wa flyovers, madaraja, reli duniani kama China lakini raia wake kila kukicha wanazamia kuja Ulaya, kila siku wanakamatwa kwenye makontena. Ukiwauliza tatizo nini ukiwa unafahamu kuwa China ni nchi tajiri kimiundombinu, watakwambia wanahitaji maisha bora na uhuru.

Sasa huyu kila siku yeye anasema anataka kuifanya Tanzania iwe kama Ulaya sijui anajua China iko Ulaya? ni bora angekuwa anasema anataka kuifanya Tanzania kuwa kama China (kitu amabacho nacho hawezi) tungekubaliana naye lakini kwa ubora wa maisha amekwishafeli.

NI WAKATI SASA WANANCHI KUCHAGUA IKIWA MNATAKA RAIS AMBAYE ATAJENGA MIUNDOMBINU AKIBORESHA MAISHA YENU PIA, AU RAIS AMBAYE KWAKE YEYE MAENDELEO NI MIUNDOMBINU PEKEE BILA KUBORESHA MAISHA HALISI YA MWANANCHI NA KUMPATIA UHURU WAKE.

Ni wakati wa kuchagua Tundu Lissu ili ujengewe miundombinu huku maisha yako na uhuru vikiboreshwa ama John Magufuli ambaye tafsiri ya maendeleo kwake yeye ni ujenzi pekee huku akiminya haki za binadamu na kufuta uhuru wa kujieleza.

Jioni njema
Miradi yote ya CCM imejaa kasoro mapungufu makubwa kuna ufisadi wa kutisha, SGR wana miezi minne hawajalipwa pesa zao, ujenzi ni wa kusuasua pesa zote amekuchua mtukufu mwenyekiti wa CCM kupeleka chato na kwenye kampeni
 
kabla ya mzungu afrika kulikua na tawala zao ambazo hakukua na haya mambo uloyataja hapa.
But ndizo zilizoshiriki kumuuza mwafrika kwa mzungu na mwarabu Kama mtumwa,pia ndizo zilizopromote slave trade iweje mwarabu anatoka Kongo anavuka kigoma Hadi bagamoyo na anapita kwenye vijiji na pana watu walishindwa vipi kuwauwa hao waarabu ili kuwakomoa waafrika wenzao,ubinafsi wa watawala wa kiafrica haukuanzia leo
 
Unawashawishi Watanzania wachague majambazi na wauza nchi...
Nchi imeuzwa chato pesa zote wamekomba Hazina kwenda kwenye kibubu chake zingine kapeleka kwenye kampeni
 
Miradi yote ya CCM imejaa kasoro mapungufu makubwa kuna ufisadi wa kutisha, SGR wana miezi minne hawajalipwa pesa zao, ujenzi ni wa kusuasua pesa zote amekuchua mtukufu mwenyekiti wa CCM kupeleka chato na kwenye kampeni
Kwani jengo la chadema limekamilika.
 
Miradi mingi mipya imeanzishwa kama sehemu ya kuzipigia Kodi zetu kuzitakatisha thus Hakuna uwazi kwenye mikataba Wala kujua risiti za ndege kujua zimenunuliwa vipi,bei gani,zimeingiza ngapi Ni mtu na mjomba wake ndo ujiamulia wengine sie kazi yetu ni kulazimishwa kulipa Kodi na sio kujua imetumika vipi
 
Tusingekuwa tunawakamata wa Ethiopia kila wa leo kwenye malori wakati wana bwawa kubwa kiliko Stiegler, wana SGR inayofanya kazi na wana shirika kubwa la ndege,moja ya mashirika makubwa sana Afrika
Kwanza miradi yote mikubwa ina ufisadi mkubwa na wanufaika wa hiyo miradi ni wanaccm
 
Kwa kweli huwa najiuliza sipati majibu j.kikwete alijenga sana miundombinu lakini watu walikuwa na maisha sio magumu kama ya huyu mshua alikuwa anafanyeje?ila inaonekana mzee baba huyu anatuibia sana haiwezekani hali iwe ngumu sana namna.watu hali ni mbaya balaa.
IMG_20200828_203405.jpeg
 
Kwani jengo la chadema limekamilika.
Majengo ya CCM ni ya vyama vyote mwaka 1991 baada ya Tanzania kutangazwa ni Nchi ya mfumo wa vyama vingi ilipaswa majengo viwanja mali za CCM vigawanywe kwa vyama vyote, chadema haiwezi kujenga jengo jipya wakati inajua majengo ya CCM ni yao.
 
Miradi yote ya CCM imejaa kasoro mapungufu makubwa kuna ufisadi wa kutisha, SGR wana miezi minne hawajalipwa pesa zao, ujenzi ni wa kusuasua pesa zote amekuchua mtukufu mwenyekiti wa CCM kupeleka chato na kwenye kampeni
Daaa jamaa anatupiga sana
 
Back
Top Bottom