Uchaguzi 2020 Mnataka tuendelee kuwa na Rais wa miundombinu? Ingekuwa miundombinu ndiyo kipaumbele cha mtu wachina wasingekamatwa kwenye makontena wakizamia Ulaya

Majengo ya CCM ni ya vyama vyote mwaka 1991 baada ya Tanzania kutangazwa ni Nchi ya mfumo wa vyama vingi ilipaswa majengo viwanja mali za CCM vigawanywe kwa vyama vyote, chadema haiwezi kujenga jengo jipya wakati inajua majengo ya CCM ni yao.
Naona hujui sheria za umiliki,mali ikiwa ni ya chama fulani maana yake ni kwamba chama ndicho kinachomiliki sio wanachama,mali za taasisi kama cha cha siasa haziwezi kugawanywa kwa wanachama walioamua kuondoka chamani,lakini kama chama kinavunjika kwa maana kinakuwa hakipo na wanachama wote wameridhia kivunjwe hapo ndio mali ugawanywa kwa taasisi mpya Zitakazoanzishwa na waliokuwa wanachama wa kile kilichovunjika ila si kwa watu,ivyo waliojitoa kwenye chama cha ccm hawawezi kupewa chochote kwa sababu chama hakikuvunjika ila wewe ulijitoa.
 
Kwa kweli MUNGU atende maana tunateseka sana na hiki chama
Awatoboi wanaogopa hasira za watz thus wanajipitisha bila kupingwa lakin haisaidii kitu,dalili za chama mfu Ni kubebwa na dola
 
we unadhani walifanya yote hayo kwa kupenda? walijaribu kupigana na hawa wavamizi bt kwa kua walikua na silaha duni ndo maana mambo yaliwaendea kombo wakasalimu amri bt hii sio sababu yakutaka tuendelee kujidharau na kujidunisha.
 
Ugumu wa maisha kwa mtu wa kawaida haujaletwa na Magufuli. Ugumu wa maisha wa Magufuli umewafika wezi, matapeli, wala rushwa kwa sababu hizo njia zimefungwa. Siku zote mnyonge hutegemea kuuza kuku, mazao, mifugo, samaki n.k. ili kukidhi matatizo yake madogo kama kununua chumvi. Kamwe maisha ya wanyonge hayategemei kipato cha kutabirika bali kipato kinachotegemea mazao ambayo hutegemea mvua.

Siyo siri, Magufuli kaziba mianya mingi ya kufuja mali za umma, matokeo yake hizo fedha hutumika kwenye maendeleo. Ni mjinga tu atasema hakuna pesa iliyookolewa tokana na mishahara hewa. Je tunajuwa kuwa tulikuwa tunakusanya kodi chini ya kiwango? Lakini sasa asilia mia kubwa ya kodi hulipwa. Meandeleo hayaletwi na kupiga siasa za matusi na kutafuta huruma bila kutuambia mikakati mbadala ambayo itaendeleza nchi.

Upinzani unataka kumng'oa Magufuli toka uraisi. Hii ni haki yao na ndiyo mategemeo ya chama chochote cha siasa. Lakini ili kumng'oa aliye kwenye madaraka ni lazima upewe hiyo ridhaa na wananchi kwa kwa kura. Ili wananchi wawapigie kura ni lazima mlete sera zenu za maendeleo ili tulinganishe na zile za Magufuli. Atakayekuwa na sera nzuri ndiyo tutamchagua. Hatuwezi kumchagua mtu anayetaka watu wa nje ndiyo wawe waangalizi wake. Hii ya dunia nzima inaona, na hiyo dunia ni ile inayotukopesha ni sera ya unyonge. Ina maana huko nje wewe umeandaliwa mikopo ambayo italipwa na sisi. Sisi hatuwezi kumchaguwa mtu anayeahidi kwenda kutembeza bakuli huko nje. Tunataka mtu mwenye sera za kuondokana na utembezaji bakuli.

Yaani nyie upinzani mmekosa mtu wa kuwa raisi ndiyo mnamuweka mtu mwenye ujuzi wa kutembeza bakuli nchi za nje. Hivi huyo mtembeza bakuli akipewa hizo fedha ana mpango gani wa namna ya kuzilipa. Au atawakabidhi madini maana sasa ndiyo tumempata muuza nchi haswa, anayejidai na uwezo wake wa kutembeza bakuli.
 
We unadhani walifanya yote hayo kwa kupenda? walijaribu kupigana na hawa wavamizi bt kwa kua walikua na silaha duni ndo maana mambo yaliwaendea kombo wakasalimu amri bt hii sio sababu yakutaka tuendelee kujidharau na kujidunisha.
 
Sasa ulipe Drs vizuri bila majengo? Well Drs na Wagonjwa bila hizo barabara unazozilaumu watafikaje hapo wanapokutana na kutibiana? Tz hamna ugumu wa maisha wa kutisha huko Ulaya unakokusifia maisha rahisi? Acha habari zisizo kuwa na uhalisia. Raisi wa miundo mbinu, Trump rais wa ukuta wa mexico?

Kiuhalisia wapi kuna ugumu wa maisha Ulaya au Afrika maana wazungu walikuwa na maisha magumu since 1800s ndio wakaja Afrika. Soma historia kwa nini wazungu walikuja Africa na wengine wakaenda Australia.

Hicho ulichoandika cha brain wash tu tunaamini Ulaya ndio kila kitu. Tz kuna wangapi wanafanya kazi 15hrs a day may be 6 days a week? Na hapo mtu aweze kusurvive tu. Viva Magu.
 
Kuna mengi sikubaliani na Magufuli ila namuunga mkono kwenye miundo mbinu. Faida za miundo mbinu watoto wetu ndo wataziona. Bila miundo mbinu maendeleo ya mtu mmoja mmoja ni vigumu kuyapata. Kwa mfano unalima nyanya iringa hazitafika daresalaam bila barabara.
Kujenga miundo mbinu ni kama wazazi kujinyima ili watoto wapate elimu nzuri. Faida zake huzioni mpaka miaka mingi ipite.
Hata wamarekani walitumia miundo mbinu miaka ya 1930 kuweka chachu ya uchumi kukua.
SGR ndiyo, stingler dam ndiyo, uwanja chato hapana. Muhimu ni miundo gani inajengwa na wapi inawekwa.

Sent from my SM-G935W8 using JamiiForums mobile app
 
Watu Kwanza washibe, pili wawe huru, miundombinu inajengeka tu,

Ndo maana hata Mzee Rungwe anakazia sana kwenye ubwabwa maharage ila watu wanashindwa kuielewa falsafa yake.

Viongozi wanapaswa wawekeze kwenye maisha ya watu kwanza kama kipaumbele namba moja then vyengine ndo vifuate.

Big up Mzee Rungwe, Lissu na Maalim Seif kwa kuliona hili.
 
"...Wanadamu wapo wenye kashukuru, na wapo wasioshukuru.
Wapo walionufaika kwa hayo wewe unaona yasiyomana.... Ndomana nasema , Hata Mungu kwa wema wake na vyote vizuri alivyoviumba, kuna manyumbu Bado yanamuona hafai."
Watakuambia bora nizaliwe mbwa ulaya
 
Naona wengi wanabeza Uzi huu ila ngoja wamchague njaa iwaume zaidi miaka mingne inayofuata akili ndoitakuja,watakumbuka nin maana ya maendeleo ya watu!mark my words akipita huyu mgombea wa CCM miaka mitano ijayo maisha tutakyoishi yatakuwa magumu zaidi
 
CreativityCode

Nimewiwa na shaka juu ya uimadhubuti wako wa afya ya akili kwakua ingekua umejitoa tu ufahamu na kubwata ulivyobwata ungeona aibu kwa kuelewa muunganiko kati ya miundo mbinu na uchumi, miundombinu na kuboresha maisha ya watu;

1. Unafhani yule Mfanya biashara Aliyekua anasafirisha tani moja ya mziko kwa 127,000/- toka au kwenda Mwanza - Bukoba na ikakarabatiwa meli na sasa anasafirisha tani moja kwa 27,000/- ataelewa hoja yako?

2. Yule aliyetakiwa kuunga unga na wafanya biashara wenziwe ili kukodi fuso ya kupeleka mzigo wake Dar au Moshi au Arusha na sasa hivi anapeleka mzigo wake stesheni na kuusafirisha kwa bei chee anaona treni ni kitu na sio ukombozi wa afya ya biashara yake?

3. Yule aliyewahi kupelekwa na toroli/bodaboda/baiskeli/machela zaidi ya kilometa 5 kwa ajili ya kupata uhuduma ya afya atakuelewa kwamba ile zahanati pale ni jengo na halijagusa maisha yake?

Vp wale walipokua wanakuja Muhimbili toka Kigoma kwa ajili ya MRI/ECHO na kujikita wanageuka ombaomba pale Muhimbili atakuelewa kwamba uboreshwaji wa huduma zile wilayani ni stori za vitu dhidi ya watu?

ZIPO BAKORA MUJARAB ZA KUICHAPA CCM NA MAGUFULI SIO HUU UTOTO MNAOLETA

Mfano
1. Mfumo wetu wa elimu bado una elemea kwenye nadharia na sio vitendo hivyo kuzalisha wasomi ambao ni mizigo mtaani na/au ni mfumo ambao unawabeba watu wenye uwezo wa kukariri na sio kuelewa, kuwabeba watu wenye kumbukumbu na kuwaacha wenye akili, kuwakumbatia wanaosomea mitihani na kuwaacha wenye vipaji?

2. Mpango kazi ni upi wa vijana wanaomaliza darasa la Saba na kidato cha nne na kufeli kwa kupata Daraja la nne ambao ndio kundi kubwa ukilinganisha na wanaokwenda kwenye vyuo mbali mbali vya taaluma na ujuzi?

3. Sanaa imejidhihirisha kwamba inaweza kuwa sehemu kubwa ya ajira kwa vijana wa kada zote wasomi na wasio wasomi, Serikali imeshindwa kuwapa mafunzo ya kuimarisha na kujitajirisha kupitia Sanaa zao.

Ninyi mnalipi mnalowaahidi sio kuwakusanya kwenye matamasha na kuwapatia fedha za kunywea bia na kuzinia kwa siku mbili Tatu Kisha wanarudi kwenye umasikini wa kuomba fedha za video au kuingia studio kurekodi.

Kuweni wabunifu sio kujikita kwenye kupinga kila kitu tuuuu!

Dr. Slaa
Alikua na hoja za Msingi na ndio maana wengi tulivutika na CHADEMA ni kweli nchi ilikua imetopea katika ufisadi na ilihitajika dawa mujarabu kwakua watu wengi walikua wamechoshwa na Hali ile.

Edward Lowassa
Alikua na mashiko ya kuboresha mifumo ya Elimu na akituambia kipaumbele chake Cha kwanza, pili na tatu ni elimu kwakua mfumo wa Elimu ni mbovu wengi tulimuelewa japo ndio Kura hazikutosha.

TUNDU LISSU
Anatusimulia namna alivyoyashinda mauti tuuu na kujikita katika kupinga kuliko kujenga...

Wasalaam
 
Ni bora tumchague Magufuli mzalendo kuliko Lissu msaliti, kibaraka, shoga, mwongo, mchonganishi, mvunja amani, kichaa, mtetea mafisadi na mabeberu.
 
Safi sana mkuu. Waambie CHADEMA waambie.
 
kuweka mazingira rafiki ili kuleta maendeleo ya watu na sio vitu.
Ko kujenga miundombinu haisahidii maendeleo???
Au kwa kukuuliza, kitu gan kinachochea sana maendeleo unaona kifanyike??
 
Kila kitu kina magumu yake, ndo maana enzi zile kila kukicha thamani ya pesa yetu ilikuwa inashuka, kazi na dawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…