Uchaguzi 2020 Mnataka tuendelee kuwa na Rais wa miundombinu? Ingekuwa miundombinu ndiyo kipaumbele cha mtu wachina wasingekamatwa kwenye makontena wakizamia Ulaya

Uchaguzi 2020 Mnataka tuendelee kuwa na Rais wa miundombinu? Ingekuwa miundombinu ndiyo kipaumbele cha mtu wachina wasingekamatwa kwenye makontena wakizamia Ulaya

Hivi suala la ajira ilani ya ccm wanalifanyia kazi kweli? Kwa maana kwa utafiti wangu uwezo wa serikali kuajiri umeshuka sana kulinganisha na kipindi cha kikwete
Uwezo wa sekta binafsi kuajiri umeshuka
 
Ethiapia inaongoza kuwa na mavitu na midege kuliko hayo anaesema ataongeza lakini leo hii kila kukicha wananchi wake wanakamatwa maharamia nchini mwao hakukaliki
Na Tanzania kuna kalika au hakukaliki?
 
Wachina mbali sana,semea waethiopia hapo. Kila leo wanakufa baharini kisa ulaya,na hapa kwetu Tanzania kila leo waethiopia wanakamatwa uhamiaji haramu wakati kwao wana metro,ndege shirika kubwa kuliko yote Africa,SGR,umeme n.k.Ila wananchi majority ni hohehahe.
 
Tunapopoteza matumaini tunatafuta sympathy
Jitu linajifanya kushabikia sijui ndege sijui maendeleo ya madaraja wakati ndege hajawahi panda na wala hana gari la kupitisha katika hilo daraja.
Harafu yeye choka mbaya mnyonge anajiita
kila aliyefanikiwa anamuona mwizi na freemason.
kama mkichagua tena mkapimwe akili maana mtakuwa mnamatatizo.
 
Mleta nyuzi na wote wanaokuunga mkono ninyi mnaakili ndogo Sana! Vichwa vyenu bado vinamaziwa ya mama zenyu!
 
Kama.hii Miundombinu haisaidii
Ujenzi w vituo vya afya havisaidii
Ujenzi wa shule hausaidii
Nidhamu ya kazi haisaidii

Basi tumchague
Rungwe tule UBWABWA tu
Au KAZI NA BATA ya Membe

Huyu wa Kesi na sheria aende tu Kisutu au Mahakamu kuu haiitaji uchaguzi hilo tumempa
 
Ethiapia inaongoza kuwa na mavitu na midege kuliko hayo anaesema ataongeza lakini leo hii kila kukicha wananchi wake wanakamatwa maharamia nchini mwao hakukaliki
Kuna nchi ina miundombinu kama Afrika Kusini. Lakini fuatilia umaskini wa wananchi, unatisha. Miundombinu kama flyover na ndege inamsaidia vipi mkulima wa nyanya kule kijijini. Kama haimsaidii tupa kule ndege badala yake tuwekeze kwenye mitaji na masoko ya mazao ya wakulima.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Acha uongo waliyokamatwa kwenye container wakitaka kuingia uingereza ni wavietnaam sio wachona.
Wenyewe wachina wameshaanika siri ya maendeleo yao ni kujenga miundombinu kwenye taifa lao. ..Halafu anakuja huyu mgojwa wa akili kibaraka lissu anasema analeta maneno ya kijinga.
 
Mleta mada unawakilisha akili zile zile za watu wanaoishi kwenye majiji makubwa, Dar, Mbeya, Mwanza na Arusha, akili za kibinafsi.

Huwezi kuelewa umuhimu wa madaraja wakati huyatumii maishani mwako.

Huwezi kuelewa umuhimu wa busisi inayojengwa kwa sababu hutakuja kupita mahali pale.

Huwezi kuelewa umuhimu wa zahanati kwa sababu Mama zako wadogo na wakubwa hawatakuja kuzitumia.

Huwezi kuelewa maana ya upanuzi wa bandari zote za nchi hii kwa sababu huna mpango wa kuja kufanya biashara ya usafirishaji nje na uagizaji wa bidhaa.

Huwezi kuelewa maana ya reli mpya ya umeme inayojengwa kwa sababu huna mpango wa kuja kusafiri kwa treni kutoka Dar mpaka Kigoma.

Huwezi kuelewa faida ya uwekezaji kwenye umeme mpaka Kenya wameshaanza kuielewa kazi ya REA.

Wewe ni wale wale wapiga kelele wa mijini waliozoea maisha ya leo leo yale ya kupata hela na kuitumia leo.

Wenye kuyaona maendeleo makubwa ya Ulaya na Marekani wanatambua kuwa miaka mingi iliyopita walikuwepo watu waliojinyima ili uzuri wa leo hii uweze kuonekana na kuleta tija.
 
Back
Top Bottom