Sipingani na Maoni yako, lakini hawa wanaojadili mpira kutwa nzima, je, wanatoa wapi pesa za kutosheleza mahitaji Yao ya kila siku? Mfano chakula. Maana Hewa NI ya bure Mwenyezi Mungu katupa bure. Je chakula? Ukweli ili uishi unahitaji Kula ata iwe mara moja Kwa siku tatu! Je, watu hawa wanatoa wapi mahitaji Yao muhimu ya kila siku? NI dhahiri hawapati mahitaji Yao bure Bali wanagharimia Kwa pesa!
Mijadala ya mpira ilikuwepo miaka yote lakini si Kwa kiwango hiki ila imepamba Moto miaka ya hivi karibuni.
Kwenye mpira kuna makundi tofauti, wako waajiriwa yaani wanaopata pesa kutokana na mpira, mfano wachezaji, viongozi, wenye viwanja, mahoteli, wasafirishaji, siku hizi kuna wenye mabanda ya kuonyesha mpira na wengineo.
Kuna wapenzi wa mpira, hawa wanatumia mpira Kama sehemu ya kupumzisha akili.