Mnawachukuliaje watu wa GNLD na Forever Living Products?

Mnawachukuliaje watu wa GNLD na Forever Living Products?

Mimi nilishawishiwa kujiunga na Power Club, kwa kumuamini huyo mtu, nikatoa laki mbili, hakurudi tena!
 
Kwanini usikae na huyo mtu aliyekufuata akueleweshe biashara inafanyikaje? Maana umekuja kuuliza humu kwa watu ambao hata hawajui biashara inaendaje unafikiri watakushauri nini?
 
Ni biashara nzuri Sana. Kama ilivyo kawaida, lazima ufanye Kazi bila kukata tamaa. Kuwa na malengo, inalipa vizuri. Mfuatilie,, upate mafunzo Yao ni Bure then fanya Kazi, Itakuwa poa.
 
I don't feel any pyramidal business...and as for other countries its illegal.ni kutokua na elimu ya kutosha hizi biashara sio stable i nafika mahala base of the pyramid hai extend tena na alieko top anabaki kua top beneficiary.
 
Waliofanikiwa zaidi wameacha ajira zao na wengine bado wanaendelea. Kuna mwengine anaona hela anayoingiza forever ni zaidi ya mshahara wake ameona bora aache ajira yake nakujikita na busness. Hela ipo lakin u have to work hard especially katika ku recruit watu, hiyo team yako lazima ifanye kazi coz isipo fanya kazi jihesabu huna chako. Ukiwa na team inayojituma hayo mafanikio makubwa utayaona. Ni busness nzuri lakini ni lazima uwe committed, sisi wengine commitment ilitushinda.
acha uongo kk
 
Nop, focus ya kwanza ni afya, mambo ya biashara yanafuata, tena ukipenda sio lazima, bt acha wanaoteseka wapate afya as you.
Tamalisa kumbe umekua busy upo na hawa matapeli? achana nao vitu ambavyo ni too much theoretical sio issue
 
Habarini wadau.

Ninaelimishwa Sana na mada zijadiliwazo humu ndani. Leo natamani kuelimishwa kuhusu membership za kampuni za gnld, forever living na nyinginezo Kama hizi.

Ni Mara ya tatu sasa wanakuja kwangu na ushawishi mkubwa kwamba kampuni hizi zitanipa faida kubwa yaani nitatoka kimaisha.

Sina wasiwasi na products zao nna wasiwasi na mafanikio makubwa wayapatao wanachama kwa kadri uongezavyo watu. Wasiwasi wangu sasa ni huu; hakuna uhusiano wa kampuni hizi na free mason? Mbona hatusikii zikijitangaza kwenye vyombo vya habari?

Kama kuna faida kubwa kuwa huko mbona basi watu wasiache ajira zao na biashara zao na kujiunga na kampuni hizo? Msaada jamani. Pesa naipenda ila zina mipaka yake
kwa uchumi wa nchi hii umuuzie mtu dawa ya meno Elf 15 sio rahis kwa hio hii ni vitu vya kufikirika tu
 
Hii ni kamari ni kama DECI tuu,haina chochote,wengi walio kwenye hii michezo wana tabu sana,utaona wamevaa vizuri lakini wanaukata wa ajabu.
Moja ya tatizo kubwa la hii mi network marketing ni kukausha pesa.Ukiwa huku unakaukiwa pesa kusiko kawaida.
Hii inatokana na kuunganishwa kishetani ktk chain yao hivyo hukunyonya riziki zako,wengi future zao zimeharibika.
 
sasa hivi kuna na rifaro,siku hizi wanapenda sana kushind fb kuunganisha watu magroup ya ujasiriamali,mtu unajiunga kubadilishana mawazo huko whatsap mara hawakawii baada ya muda kuanza mambo yao,kuna siku jamaa aliuliza rifaro si imefungiwaa,mi nikajibu zimekaa kitapel daah sikumaliza dr admin akanitoa yani nilicheka sana daah eti akanijibu private kuna watu wameshawekeza hela zao nisiwaharibie,sasa si utapeli huu
 
HABARI ZENU WANDUGU.

kichwa tajwa chahusika,,hili swala la biashara za mitandao e.g. foleverliving n.k zimeshamili sana mjini, lakini kila mara nimekuwa nikikaribishwa na rafiki zangu waliojiunga, binafsi sijawahi kushawishika naona kuna ugumu kutengeneza chain,

kilichonisukuma kuandika huu uzi , juzi kati tena jamaa mmoja kanikaribisha pale mitaa ya posta mpya, kwenye biashara zilezile, tofauti kabisa na nilivyozoea kusikia wao wanasema kiingilio ni USD 2000(5M tsh).swali langu ni kwamba inawezekana kweli kuludisha hyo hela ukichukulia biashar hii kwa sasa kila mtu anaijua??.

ebu wataalamu nipeni uzoefu kabla sijaibiwa 5m.

asante,
 
Ni mashirika mazuri sana ukitaka kutajirika jiunge huko
 
Wakati nipo chuo kuna rafiki yangu mmoja mjasiriamali (mangi ) baada ya kupokea bumu lake, akapeleka Forever Living Products laki sita yote. Kilicho mtokea kinasikitisha, ilibidi hizo dawa aanze kuzitumia mwenyewe kwa kuzinywa.. Semester ilikuwa ngumu sana kwake, ashukuru Mungu alikuwa anasoma BAGEN ila vinginevyo angeliwa kichwa..sasa hivi hataki kabisa kusikia kitu chochote kile kinachoitwa FLP au GNLD


Dah! Nimejikuta nacheka saaana ....Hawa watu si wazuri kabsaaa ..Yaani usipende kuwa no jirani ukiwa na mpango wa kupata kiasi cha pesa maana zote utazipeleka huko..Ukizingatia usawa huu cjui!!!
 
Dah! Nimejikuta nacheka saaana ....Hawa watu si wazuri kabsaaa ..Yaani usipende kuwa no jirani ukiwa na mpango wa kupata kiasi cha pesa maana zote utazipeleka huko..Ukizingatia usawa huu cjui!!!
Its all a pyramid scheme!
 
Back
Top Bottom