Mnawafahamu waliompachika Dkt. Salim Ahmed Salim jina la Hezbollah katika kugombea Madaraka?

Bro, tuanze na wewe na boriti lako jichoni kwako, je unajua kuwa wewe ni mdini? Au hujui
 
..Je,habari kwamba Salim Ahmed Salim alikataa kuwa Makamu wa Raisi baada ya Dr.Omar Ali Juma kufariki ni kweli?

..kuna habari nyingine kwamba Salim A Salim aliombwa na Mwalimu arudi kugombea Uraisi mwaka 1995 wakati Mzee Mwinyi amemaliza muda wake lakini Salim akasita.

..kama ni kweli habari hizo ni kweli basi kilichomkosesha Uraisi Salim Ahmed Salim ni kigugumizi chake cha kupokea fursa za kisiasa zilizomtokea.
 
Hatari sana!! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hizi ndio yale yale mastori ya mjini, ni uongo mtupu huu.
 
alikuwa Mr yes mzee! Watu wa hivo ni hatari sana.
Hautasogea kimaslahi utadumaa!

Waongo.
wanafiki.
roho mbaya
Wachawi
Wezi
Majungu
ndo wazuri hao unapata changa moto.
Km yusufu asingeuzwa na watu wenye roho mbaya tungekuwa bado tuko middle east.
 
Salim alikuwa kijana Sana wakati anaanza siasa..
Kumbuka anaenda kuwa Balozi Misri ana miaka 18 Tu ndo akaenda kusoma huko huko..

Alipaswa kuandika historia yake..
Alikuwa anapigwa vita na wengi
Nyota yake iling'aa mapema sana
 
Salim alikuwa mwanachama Afro Shirazzi Party ujana wake. Uarabu wake umekuwa "liability". Wabaguzi ,CCM ZNZ wanasema mtoto wa nyoka ni nyoka tu.
 
Mi navojua !ukishatoa kitabu cha historia ya maisha yako ujue kifo kinafuata!!!
Halafu jk hakuwa sawa coz alijua mechi itaahirishwa badae!!halafu yeye ndio alishauri mechi isogezwe mbele!alicheza boko usipime!!!
 
kwanini Nyerere alimpendekeza Ali Hassan kwasababu alikuwa na khofu kwamba Zanzibar itapata maendeleo sana nchini ya Ali Hassan na Seif Sharif hiyo ndio sababu ya Nyerere kumpendekeza Ali Hassan mwinyi kutoka Mkuranga
 
Ahmed Salim alikua kiongozi mwenye nidhamu na mwanamapinduzi. Nadhani hii ilimfanya kutokua na ubinafsi kiasi cha kukaa kimya adui zake walipomfanyia hila.
 
Ali Hassan Mwinyi ni mnufaika wa ghiliba, fitina na mizengwe ya kutisha dhidi ya Dr Salim Ahmed Salim, rejea mchakato wa kumpata mrithi wa Mwalimu Nyerere alipong'atuka 1985 utanielewa!
 
Na mwinyi ndiye alimtengenezea njia kikwete kwa kumbeba kwa mambo mengi
Ali Hassan Mwinyi ni mnufaika wa ghiliba, fitina na mizengwe ya kutisha dhidi ya Dr Salim Ahmed Salim, rejea mchakato wa kumpata mrithi wa Mwalimu Nyerere alipong'atuka 1985 utanielewa!
 
Dr Salim alitifuana na Wamarekani pale alivyopiga kura UN kuisaidia China mpaka Ronald Reagan akawakashifu Waafrika na kuwaita manyani


Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…