Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
hiyo hali kitaalamu inaitwa kukolea, yaani mahusiano au ndoa imekolea🐒Ndugu zangu habari za weekend wakuu
Kuna wakati mwanaume hutaki kukaa nyumbani kukwepa makelele ya mwanamke na maneno mengi yasiyo na mpango. Ila kuna kipindi mwili na akili vinachoka kudhurura vinaona bora upumzike nyumbani kwako hata kidogo kuliko kwenda bar, kijiwe au kukodi lodge ili kulala mchana
Shida inakuja umeamua kupumzika nyumbani ila sasa ni kelele, maneno yasiyo na mpangilio mara lawama za kila aina na ukiamua kukaa kimnya huku umejilaza kitandani atajifanya anapangua kabati akunje nguo na kuzitupia kitandani kusudi tuu akukere.
Je, wakuu mnawezaje kuyashinda haya majaribu na kuishi na mwanamke wa design hii ujizingatia ukisema ufukuze uishi na mwingine utafukuza wengi sana ndugu zangu
Mm kushinda nje ya nyumba yangu wakati mwingine siwezi naona nateseka zaidi
apo sasa ndio real love inapaswa ku-emerge, kuonekana na kuchukua nafasi yake bayana.
ustahimilivu, subra na msamaha ndio njia pekee ya kutoka kwenye kukolea huko pazito, ambako unaweza hisi kama mkwamo ama mkosi 🐒
Imeandikwa,
Pale Ninapokua Dhaifu Ndipo Nilipo na Nguvu ...
ni wako huyo ng'ang'ana nae taratibu mtafika mbali salama🐒