Mnawezaje kuishi na watu wanaowaambia mama zao kila kitu kuhusu wenza walionao?

Mnawezaje kuishi na watu wanaowaambia mama zao kila kitu kuhusu wenza walionao?

Me too

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2015
Posts
7,388
Reaction score
9,333
Mliwezaje kuishi na hawa wakuitwa mtoto wa mama?

Yaani mnachopanga mama anakijua, mkikutana mama anajua, mkisimuliana background mama anajua, ukiomba hela mama anajua tena anaomba ushauri kwa mama kwanza kabla ya kukupa hela, mkikorofishana mama anajua, mkipatana mama anajua ukiumwa ukimwambia mama ashajua.

Naweza kusema sio mbaya ila mama akoshajua haishii hapo huwa anampa na conclusion kabisaaa. Yaani huyo mtoto wa mama anaishi maisha ya mama sio yake. Yote mzungumzayo hufika kwa mama si kwamba hana kifua ni kulemazwa kuwa mama ampe tecnic za kuishi na mwenza wake.

Mbaya zaidi mama huyu naye umri ukipita wa kustaafu halafu ujana wake aliutumia kujipamba, mawigi na kuoshwa miguu na vijana wapaka rangi akistaafu pesa hupungua, mwanae ndiye anayekuwa ajira mpya ya kutimiza mapungufu.
sasa mama huyu kamseti mtoto toka awali na mtoto nae ndiyo hivyo mambo yote mama anayo, uhusiano huo utasonga mbele kweli?

Hebu mtupe ujuzi namna ya kuishi kwenye mahusiano na hawa watoto wa mama.

KARIBUNI.
 
Ukitaka kuishi nao vizuri uwe na hela zako lakini ukitegemea hela zake usikasirike hata mama yake ana haki nazo.
Upande wa pesa elimu hii wanawake tumepewa mda sana kiasi kwamba sizani km kuna mwanamke,anategemea pesa ya mwanaume 100%

Shida maamuzi yanatoka kwa mama sio kichwa yake.
 
Hapo kazi unayo..... Mana unatumikia ndoa mbili ya Kwanzaa mama yake anqtakiwa akupende akikuchukia tuu ndoa Huna ya pili ni yeye.....

Wana ume wa hivi ili uwe salama ni akupende Sana Ile hawez kukuaacha ndio salama yako Kuna baadhi ya maamuzi atashidwa kufanya kama kukuaacha kwa sababu rahisi ambazo Mala nying zawesa tengenezwa na mama mkwe be strong muda ukifika atabadilika ingawa kwa kuchelewa
 
Mpaka akae sawa si ndo mtihani
 
Back
Top Bottom