Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa huyo mtoto wa mama ni kulapua makofi tu ili akaseme tena kwa mama yake.kwa mfano mwanaume anapigwa makofi eti?
Dàh, kazi kwelikweliee halafu sie kwetu tuna mangombe ndizi mama huwekeaga nyama ya ngombe ya maana.😂
Maisha ya hivyo hayana mwisho mzuriUkitaka kuishi nao vizuri uwe na hela zako lakini ukitegemea hela zake usikasirike hata mama yake ana haki nazo.
shida huyu mtoto wa mama atengenezejww ili aelewe anatakiwa ajitegemee kiakili, kimaamuzi, kifikra na hata kiuchumi?Una kazi kubwa sana...yaani mama akikuchoka ni anatoa order tu uachwe na sababu jamaa yako hana kichwa cha kujitegemea atakufukuza ukute tayari na watoto mnao.
Yaani hapo ni ujitajidi kumnyenyekea mama mkwe nje ya Hapo unalo.
Aisee ni kazi sana sikukatishi tamaa lakini Nina ushuhuda wa watu wa aina hiyo ambao walishindwa kubadilika kabisa hasa pale unapotofautiana na mama yake.shida huyu mtoto wa mama atengenezejww ili aelewe anatakiwa ajitegemee kiakili, kimaamuzi, kifikra na hata kiuchumi?
Mliwezaje kuishi na hawa wakuitwa mtoto wa mama?
Yaani mnachopanga mama anakijua, mkikutana mama anajua, mkisimuliana background mama anajua, ukiomba hela mama anajua tena anaomba ushauri kwa mama kwanza kabla ya kukupa hela, mkikorofishana mama anajua, mkipatana mama anajua ukiumwa ukimwambia mama ashajua.
Naweza kusema sio mbaya ila mama akoshajua haishii hapo huwa anampa na conclusion kabisaaa. Yaani huyo mtoto wa mama anaishi maisha ya mama sio yake. Yote mzungumzayo hufika kwa mama si kwamba hana kifua ni kulemazwa kuwa mama ampe tecnic za kuishi na mwenza wake.
Mbaya zaidi mama huyu naye umri ukipita wa kustaafu halafu ujana wake aliutumia kujipamba, mawigi na kuoshwa miguu na vijana wapaka rangi akistaafu pesa hupungua, mwanae ndiye anayekuwa ajira mpya ya kutimiza mapungufu.
sasa mama huyu kamseti mtoto toka awali na mtoto nae ndiyo hivyo mambo yote mama anayo, uhusiano huo utasonga mbele kweli?
Hebu mtupe ujuzi namna ya kuishi kwenye mahusiano na hawa watoto wa mama.
KARIBUNI.