Mnazipendea nini hidden roof house?

Hapa jirani kuna nyumba ziko kwenye gate moja za kupanga mwenye nazo anaishi marekani. Ni nyumba mbili nzuri moja ina hidden roof. Aisee anayeishi anadai kila mvua ikinyesha na kazi ya kudeki ndani maji yanaingia. Ashamwambia mwenye nayo na imefanyiwiwa marekebisho zaidi ya mara tatu lakini tatizo haliishi. Ni nyumba nzuri kweli yani ila ndio changamoto hiyo.
Nadhani kama ulivyosema, tatizo mafundi wetu kila fundi hujifanya anaufahamu wa kila kitu.
 
Alafu mbona kama hazirekebishiki jumla, wengi wanaorekebisha baada ya muda tatzo linajirudia.
 
Yangekuwa mabanda hata wewe ungejenga,isingekuwa big agenja mjini.
Nimejenga lakini siyo hayo madude. Ngoja nikutoe ushamba. Kuna roofing styles mbalimbali. Moja ni flat roof. Hizi zipo toka enzi za biblia, na watu waliweza kukwea na kupumzika huko. Sasa mtu akikudizainia nyumba ya flat roof na kuiita contemporary(Ya kisasa) ujue amekuona zoba sana.
 
Nimepitia comment ya kila mtu, mimi ni mhanga wa hii kitu, bahati ni vile ameezeka hivi juzi na mvua hizi kubwa zikaanza. Dah aisee jumba linavuja ni hatari, alimimina zege kali sana lakini bado. Nilichiwaza kichwani mwangu:
1. Nitafute sheets special litakalokunjwa na kuchomelewa hadi pale mabomba ya kumwaga.
2. Nifunge gata hadi zilekeze maji kwenye mabomba ya kutolea maji nje
3. Mjenzi mwenyewe anasema ataongeza slop na kuweka tiles
 
Mkuu,
Fundi anaepaua ashindwe kugonga bati kweli?
Mafundi wengi wamekuwa multipurpose, multitasking wanafanya mambo mengi ila umakini ni muhimu. Atapandisha boma, atasema anaweza kupaua unampa kazi, atasema blundering umuachie, atasema umpe plastering, hadi kufunga board. Usipokuwa makini unaingizwa chaka.
 
1. Nenda Nabaki Afrika wana materials special kwa ajili ya joints, wana gundi maalumu na hizo sheets pia.
2. Option ya tiles achana nayo, it's not a solution.
 
Huna uwezo wa kujenga contemporary,utaishia kujenga pitched roof za maskini

Mengine ni kujifariji tuu.
 
Kila kitu unajua sio visima, nyumba, utabiri wa hali ya hewa😂wewe mchina au
 
Kaka Glenn naomba kiramani simpo cha vyumba vinne , dinning , jiko na kila chumba self contained
 
Ingekua watu wanaonekana mazoba kila mtu angekua nayo

Nyumba sio matako kila mtu anayo
 
Mafundi wengi hawana ujuzi nao bado
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…