Mnazipendea nini hidden roof house?

Mnazipendea nini hidden roof house?

Ni nyumba za kisasa lakini bado hatuna mafundi wazuri wa kuweza kuzifanya ziendane na hali zote, zimekuwa ni nyumba nzuri sana kipindi cha kiangazi, kipindi cha mvua nyingi ni majanga matupu zinavuja mno lakini bado watu wanajenga sana nyumba kwa mtindo huo ambao sio rafiki hasa kipindi cha mvua.

Kuna mwenye nyumba hapa kila ikinyesha mvua lazima umuone fundi kapanda juu ya bati(navyotype tayari kuna fundi juu ya bati) na wapangaji wake wanalalamika sana maji kuingia ndani na kulowanisha vitu. Kila akiendelea kujenga style ni hiyo hiyo lawama nyingi akiziangushia kwa mafundi wake.

Mafundi upi ushauri wenu juu ya hili?
Upi ni mtindo mzuri wa kupaua nyumba kwa mazingira ya huku kwetu na aina ya mafundi tulionao mitaani?
View attachment 2805821
Hapa jirani kuna nyumba ziko kwenye gate moja za kupanga mwenye nazo anaishi marekani. Ni nyumba mbili nzuri moja ina hidden roof. Aisee anayeishi anadai kila mvua ikinyesha na kazi ya kudeki ndani maji yanaingia. Ashamwambia mwenye nayo na imefanyiwiwa marekebisho zaidi ya mara tatu lakini tatizo haliishi. Ni nyumba nzuri kweli yani ila ndio changamoto hiyo.
Nadhani kama ulivyosema, tatizo mafundi wetu kila fundi hujifanya anaufahamu wa kila kitu.
 
Alafu mbona kama hazirekebishiki jumla, wengi wanaorekebisha baada ya muda tatzo linajirudia.
 
Yangekuwa mabanda hata wewe ungejenga,isingekuwa big agenja mjini.
Nimejenga lakini siyo hayo madude. Ngoja nikutoe ushamba. Kuna roofing styles mbalimbali. Moja ni flat roof. Hizi zipo toka enzi za biblia, na watu waliweza kukwea na kupumzika huko. Sasa mtu akikudizainia nyumba ya flat roof na kuiita contemporary(Ya kisasa) ujue amekuona zoba sana.
 
Nimepitia comment ya kila mtu, mimi ni mhanga wa hii kitu, bahati ni vile ameezeka hivi juzi na mvua hizi kubwa zikaanza. Dah aisee jumba linavuja ni hatari, alimimina zege kali sana lakini bado. Nilichiwaza kichwani mwangu:
1. Nitafute sheets special litakalokunjwa na kuchomelewa hadi pale mabomba ya kumwaga.
2. Nifunge gata hadi zilekeze maji kwenye mabomba ya kutolea maji nje
3. Mjenzi mwenyewe anasema ataongeza slop na kuweka tiles
 
Huwezi kutumia fundi mmoja nyumba nzima kuna mambo mengi mfano wa kuanzisha boma hawezi kupaua na kuna wengine wa kupaua hawezi kugonga bati

Hata ukimtumia contractor kukosoana kupo pale pale kiufupi nyumba hadi inaisha ikawa na kasoro ndogo mshukuru Mungu
Mkuu,
Fundi anaepaua ashindwe kugonga bati kweli?
Mafundi wengi wamekuwa multipurpose, multitasking wanafanya mambo mengi ila umakini ni muhimu. Atapandisha boma, atasema anaweza kupaua unampa kazi, atasema blundering umuachie, atasema umpe plastering, hadi kufunga board. Usipokuwa makini unaingizwa chaka.
 
Nimepitia comment ya kila mtu, mimi ni mhanga wa hii kitu, bahati ni vile ameezeka hivi juzi na mvua hizi kubwa zikaanza. Dah aisee jumba linavuja ni hatari, alimimina zege kali sana lakini bado. Nilichiwaza kichwani mwangu:
1. Nitafute sheets special litakalokunjwa na kuchomelewa hadi pale mabomba ya kumwaga.
2. Nifunge gata hadi zilekeze maji kwenye mabomba ya kutolea maji nje
3. Mjenzi mwenyewe anasema ataongeza slop na kuweka tiles
1. Nenda Nabaki Afrika wana materials special kwa ajili ya joints, wana gundi maalumu na hizo sheets pia.
2. Option ya tiles achana nayo, it's not a solution.
 
Nimejenga lakini siyo hayo madude. Ngoja nikutoe ushamba. Kuna roofing style mbalimbali. Moja ni flat roof. Hizi zipo toka enzi za biblia, na watu waliweza kukwea na kupumzika huko. Sasa mtu akikudizainia nyumba ya flat roof na kuiita contemporary(Ya kisasa) ujue amekuona zoba sana.
Huna uwezo wa kujenga contemporary,utaishia kujenga pitched roof za maskini

Mengine ni kujifariji tuu.
 
Mkuu,
Fundi anaepaua ashindwe kugonga bati kweli?
Mafundi wengi wamekuwa multipurpose, multitasking wanafanya mambo mengi ila umakini ni muhimu. Atapandisha boma, atasema anaweza kupaua unampa kazi, atasema blundering umuachie, atasema umpe plastering, hadi kufunga board. Usipokuwa makini unaingizwa chaka.
Kila kitu unajua sio visima, nyumba, utabiri wa hali ya hewa😂wewe mchina au
 
Labda nikupe siri;

Contemporary haitakiwi ijengwe na fundi tena fundi Maiko.
Ikiwa unatumia fundi hskikisha una Consultant.

Kazi ya roofing huanza kuandalia kuanzia ujenzi wa msingi.

#Ninarudia# roofing ya contemporary huanza huandaliwa kuanzia ujenxi wa msingi.

××××kuna kitu tunaita Duct×××

Huu ni uwazi maalum unatumiwa kwa ajili ya kushushia maji kutoka kwa paa.

So inaanza kwenye msingi.

Kwa ghorofa duct ni uwazi unatumika kupitishia mabomba ya maji machafu, umeme nk.

Kwa contemporary ni maalum kwa kushusha maji.

Ujenzi wa contemporary ni rahisi sana na gharama nafuu.

Note: ukisha jenga boma bila mshauri/consultant eti ukatafuta fundi wa roofing, uandae na mbegu za samaki kabisa
Kaka Glenn naomba kiramani simpo cha vyumba vinne , dinning , jiko na kila chumba self contained
 
Nimejenga lakini siyo hayo madude. Ngoja nikutoe ushamba. Kuna roofing style mbalimbali. Moja ni flat roof. Hizi zipo toka enzi za biblia, na watu waliweza kukwea na kupumzika huko. Sasa mtu akikudizainia nyumba ya flat roof na kuiita contemporary(Ya kisasa) ujue amekuona zoba sana.
Ingekua watu wanaonekana mazoba kila mtu angekua nayo

Nyumba sio matako kila mtu anayo
 
Nimepitia comment ya kila mtu, mimi ni mhanga wa hii kitu, bahati ni vile ameezeka hivi juzi na mvua hizi kubwa zikaanza. Dah aisee jumba linavuja ni hatari, alimimina zege kali sana lakini bado. Nilichiwaza kichwani mwangu:
1. Nitafute sheets special litakalokunjwa na kuchomelewa hadi pale mabomba ya kumwaga.
2. Nifunge gata hadi zilekeze maji kwenye mabomba ya kutolea maji nje
3. Mjenzi mwenyewe anasema ataongeza slop na kuweka tiles
Mafundi wengi hawana ujuzi nao bado
 
Back
Top Bottom