Mnazipendea nini hidden roof house?

Hutumii gharama kubwa kwenye bati zinaenda chache
Halafu hii style niya toka zaman yaan tumezaliwa tumezikuta nyumba za hivyo
na nyumba haivuji
Baadhi ya Mafundi wa sasa ni midosho tu
Nyumba za zamani walijitahidi kuweka slope kwenye bati tofauti na sasa hivi slope wanailaza sana ndio maana bati linavunjwa kwasababu maji yanashindwa kufloor
 
Naona wanatandika majamvi na magunia juu halafu wanapaka rangi

Mbona nchi zingine zipo sana na mvua zinanyesha kama kwenu?
Ujanja ujanja mwingi waswahili ndio maana wanalalamika ooh kwanini eti usalama 😄 hawadhibiti bidhaa za Kenya

Wajerumani wanatengeneza nyumba kiwandani wewe wanakupakilia kwenye meli au malori unakuja kufungiwa kila kitu
Kama unavyofungiwa boda.
 
Huu uzi ni kama umenilenga mimi,lakini kwa kua ulikua ujenzi wangu wa Kwanza sijilaumu nimejifunza.

Lakini Kamwe sitojenga Dream House nifanye Hidden Roof, ukweli ni heri umwage Slab huko juuu kama wewe shida ni hutaki kuona BATI.

Lakini kujenga hidden roof tusidanganyane hizi nyumba za hivi si za kuishi mwanadamu ni special kwa wanyama wafugwao.

Aseee nimefumua Gypsum zote kwasababu zimeloa zimeshuka chini, hii hasara sitoisahau ila nimekoma na sirudiiii.

Hata uje uniambie wewe ni fundi uliebobea umesomea chuo bora duniani cha ufundi, Hunishawishi kuhusu Hidden Roof nikakuelewa.
 

Mtu anakuwekea bati badala ya zege ushaona wapi 😁 hii style ipo duniani kweli!! Kama ushawahi kufika nchi za kiarabu wanatumia zege, tena ya uhakika acha za huku kwetu uchanganyaji wa cement/kokoto ni majanga, mara uibiwe cement na nondo dah 😁 japo sio wote wenye hiyo tabia mbaya
 

Pole sana mkuu
 
Hutumii gharama kubwa kwenye bati zinaenda chache
Halafu hii style niya toka zaman yaan tumezaliwa tumezikuta nyumba za hivyo
na nyumba haivuji
Baadhi ya Mafundi wa sasa ni midosho tu
Si ndio hapo.nenda mikoa yote tanzania mahal mji umeanzia utakuta nyumba za bati kuficha ila wao walikua wanaacha nyuma inamwaga so slope inaanzia mbele. Mchezo wa mafund mmmoja kaja anasema hapa kwenye mferej wa kukusanyia maji piga tiles .utaalam wa wap huu? Solutions mwaga slope upande mmoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…