Mnazipendea nini hidden roof house?

Mnazipendea nini hidden roof house?

Vitu kama hivi lazima uweke, kati ya bati na ukuta. Wengi wanachimbia tu bati linaingizwa kwa ndani, anasema cement kali inatosha, anachanganya na waterproof akidhani inatosha. Lazima uchezee dimbwi la maji ndani
Screenshot_20230825_184346_Facebook.jpg
 
Humu kila fundi sio fundi maiko muite uone,,,,

Nilichoona kwenye ujenzi kila fundi anamkosoa mwenzie unakuta umejenga nyumba ukamtumia fundi mmoja hadi kwenye lenta ukichukua mwingne cha kwanza anaanza kukosoa kazi ya mwenzie

Maana ya kumkosoa mwenzie ili umuone yeye anajua kuliko mwingine mwisho wa siku nayeye anatengeneza atakapoishia ukichukua mwingne anamkosoa alopita

Mafundi ni pasua kichwa sanah
Sio mbaya kumpa contractor akusimamie kazi Yako mwanzo mwisho,hii ya kubadilisha mafundi ndio Ile nayo Ina leta shida mwishoni ,ni vile tu hela zenyewe sometimes tunaungaunga
 
Sio mbaya kumpa contractor akusimamie kazi Yako mwanzo mwisho,hii ya kubadilisha mafundi ndio Ile nayo Ina leta shida mwishoni ,ni vile tu hela zenyewe sometimes tunaungaunga
Contractor anafanya budget inakuwa kubwa ila anakupa kitu kizuri coz usimamizi unakuwa wa kuaminika. Unaweza ku-opt engineer/site foreman mwenye mishe zake akusaidie usimamizi kwa gharama za kizalendo. Anakuja asubuhi, anawaelekeza mafundi na kusepa zake, mchana anakuja kukagua kazi..like that. Ila full time contractor ujipange.
 
Sio mbaya kumpa contractor akusimamie kazi Yako mwanzo mwisho,hii ya kubadilisha mafundi ndio Ile nayo Ina leta shida mwishoni ,ni vile tu hela zenyewe sometimes tunaungaunga
Huwezi kutumia fundi mmoja nyumba nzima kuna mambo mengi mfano wa kuanzisha boma hawezi kupaua na kuna wengine wa kupaua hawezi kugonga bati

Hata ukimtumia contractor kukosoana kupo pale pale kiufupi nyumba hadi inaisha ikawa na kasoro ndogo mshukuru Mungu
 
Ni Kweli Huwezi mtumia fundi mmoja kwenye nyumba nzima,maana kila mmoja ana utaalam wake,lakini kumbuka kutumia contractor faida yake Ile ni team Moja,tofauti na Ile mchimba msingi katokea kibada,mpandisha boma katoka bahi, roofing kafanya sijui nani,,yaani nyumba ikishakuwa na mikono mingi kasoro hazikwepiki japo sijasema ukimpa contractor ndio itakuwa 100perc perfect.
 
Contractor anafanya budget inakuwa kubwa ila anakupa kitu kizuri coz usimamizi unakuwa wa kuaminika. Unaweza ku-opt engineer/site foreman mwenye mishe zake akusaidie usimamizi kwa gharama za kizalendo. Anakuja asubuhi, anawaelekeza mafundi na kusepa zake, mchana anakuja kukagua kazi..like that. Ila full time contractor ujipange.
Basi hata huyo foreman atafaa Kikubwa usimamizi tupate kitu bora
 
Naona wqnatandika majamvi na magunia juu halafu wanapaka rangi

Mbona nchi zingine zipo sana na mvua zinanyesha kama kwenu?
Ujanja ujanja mwingi waswahili ndio maana wanalalamika ooh kwanini eti usalama 😄 hawadhibiti bidhaa za Kenya

Wajerumani wanatengeneza nyumba kiwandani wewe wanakupakilia kwenye meli au malori unakuja kufungiwa kila kitu
Kama unavyofungiwa boda.
Sijaelewa paragraph ya mwisho, nyumba inajengwa huko inakuja kufungwaje huku? Au ni vyuma tu?
Huu uzi ni kama umenilenga mimi,lakini kwa kua ulikua ujenzi wangu wa Kwanza sijilaumu nimejifunza.

Lakini Kamwe sitojenga Dream House nifanye Hidden Roof, ukweli ni heri umwage Slab huko juuu kama wewe shida ni hutaki kuona BATI.

Lakini kujenga hidden roof tusidanganyane hizi nyumba za hivi si za kuishi mwanadamu ni special kwa wanyama wafugwao.

Aseee nimefumua Gypsum zote kwasababu zimeloa zimeshuka chini, hii hasara sitoisahau ila nimekoma na sirudiiii.

Hata uje uniambie wewe ni fundi uliebobea umesomea chuo bora duniani cha ufundi, Hunishawishi kuhusu Hidden Roof nikakuelewa.
Pole sana mkuu acha inyeshe tuone panapovuja
Kwa uzoefu wangu mdogo nilioupata katika kusimamia ujenzi,
Huyu style inakula bati chache, tofauti na migongo ya tembo.

Ni style nzuri sana ukimpata fundi mzuri,,
Ila fundi wa kuunga unga ni hatari.
Mafundi bado ni kizungumkuti kwenye style hii
Ujenzi unahitaji 'ufahamu' wa mambo, sio ukanjanja. Mafundi wengi hawana ufahamu wa mambo mengi sana, kwenye ujenzi unahitaji kupata ufahamu kabla ya kufanya lolote.
Mafundi ni kipengele
 
Mtu anakuwekea bati badala ya zege ushaona wapi 😁 hii style ipo duniani kweli!! Kama ushawahi kufika nchi za kiarabu wanatumia zege, tena ya uhakika acha za huku kwetu uchanganyaji wa cement/kokoto ni majanga, mara uibiwe cement na nondo dah 😁 japo sio wote wenye hiyo tabia mbaya
Kibongo bongo fundi baadhi ya mafundi bila kukuibia kazi haiendi kabisa, na ukiwa ukauki site ndio watafanya hata kusudi upate loss 😂
 
Sijaelewa paragraph ya mwisho, nyumba inajengwa huko inakuja kufungwaje huku? Au ni vyuma tu?

Pole sana mkuu acha inyeshe tuone panapovuja

Mafundi bado ni kizungumkuti kwenye style hii

Mafundi ni kipengele
Ni prefab au prefabricated houses
Wewe unapewa plan kutengeneza foundation tu na vingine vyote wanatengeneza wao na wanakuja kufunga mpaka umeme na mabomba
Unaweza kuangalia prefab house utapata idea
Ila wqna nyumba nzuri sana na wao wanakuja kukujengea au kupachika kila kitu mpaka madirisha na milango
 
Back
Top Bottom