Mnazipendea nini hidden roof house?

Mnazipendea nini hidden roof house?

Nyumba ya aina hii usijenge kama una hela ya mawazo...... utanishukuru
wenye hela za mawazo wengi wanakimbilia kujenga hizi kupunguza gharama ila baadae gharama zinazidi.
Yaani umeongea maneno ya kiufundi mpaka mimi nimstameza kuna sehemu wanajenga nimepita nikamuuliza fundi vipi hapo ushaweka duct au bado?

Ameishia kunitolea macho mimi ninayemuuliza hata mie sielewi ila kikubwa wajue na mimi najua kidogo mambo ya ufundi .
Lazima jicho limtoke na unakuta hajui kweli.
Hizi nyumba zinawatesa wengi sana,kuna nyumba moja nilipelekwa na dalali,yani mpaka nilimuonea huruma mwenye nyumba,ni nyumba kubwa vyumba 3,master bedroom safi,jiko,choo na stoo ndani,iko fenced na pavements za kutosha,lakini kila chumba ukiangalia juu gypsum zimelowana vibaya...
Nmecheka ila nimemuonea huruma mwenye nyumba, nyumba za hivyo zipo nyingi tu nyumba nzuri ila ndani kipindi cha mvua hakukaliki. Hapo labda ampangishie wa kuja asiejua kusoma mazingira na kipindi cha mvua ni ugomvi na mpangaji.
 
Ni prefab au prefabricated houses
Wewe unapewa plan kutengeneza foundation tu na vingine vyote wanatengeneza wao na wanakuja kufunga mpaka umeme na mabomba
Unaweza kuangalia prefab house utapata idea
Ila wqna nyumba nzuri sana na wao wanakuja kukujengea au kupachika kila kitu mpaka madirisha na milango
Utofauti wao ni upi hasa kwenye gharama mpaka nyumba kukamilika?
 
Utofauti wao ni upi hasa kwenye gharama mpaka nyumba kukamilika?
Mkuuu kwanza inabidi uende kiwandani halafu unachagua unachotaka yaani kila kitu mpaka tiles
Gharama zinapishana ila gharama za kusafirisha na mitambo mikubwa ya kunyanyua hizo panels zote na kama ni gorofa moja ndio zaidi

Ila watu wanajenga za hivyo na ni nzuri sana na haraka
Zipo za ghali sana Kama za vioo vitupu au eco friendly homes hizo ziko juu zaidi

Natamani kujenga eco home na kujitegemea kila kitu hata maji yajisafishe na kutumika tena
 
Labda nikupe siri;

Contemporary haitakiwi ijengwe na fundi tena fundi Maiko.
Ikiwa unatumia fundi hskikisha una Consultant.

Kazi ya roofing huanza kuandalia kuanzia ujenzi wa msingi.

#Ninarudia# roofing ya contemporary huanza huandaliwa kuanzia ujenxi wa msingi.

××××kuna kitu tunaita Duct×××

Huu ni uwazi maalum unatumiwa kwa ajili ya kushushia maji kutoka kwa paa.

So inaanza kwenye msingi.

Kwa ghorofa duct ni uwazi unatumika kupitishia mabomba ya maji machafu, umeme nk.

Kwa contemporary ni maalum kwa kushusha maji.

Ujenzi wa contemporary ni rahisi sana na gharama nafuu.

Note: ukisha jenga bomba bila mshauri/consultant eti ukatafuta futa wa roofing, uandae na mbegu za samaki kabisa
Injinia umefunguka vyema kabisa, hapo kwenye Note fafanua zaidi kuna kitu kama nimeelewa hivi alafu kama sijaelewa.
Swali, hivi huwezi kumuwajibisha fundi kwa ishu kama hii?
 
Mkuuu kwanza inabidi uende kiwandani halafu unachagua unachotaka yaani kila kitu mpaka tiles
Gharama zinapishana ila gharama za kusafirisha na mitambo mikubwa ya kunyanyua hizo panels zote na kama ni gorofa moja ndio zaidi

Ila watu wanajenga za hivyo na ni nzuri sana na haraka
Zipo za ghali sana Kama za vioo vitupu au eco friendly homes hizo ziko juu zaidi

Natamani kujenga eco home na kujitegemea kila kitu hata maji yajisafishe na kutumika tena
Nmekuelewa shukrani mkuu.

Kama uchumi unaruhusu jenga mkuu.
 
Humu kila fundi sio fundi maiko muite uone,,,,

Nilichoona kwenye ujenzi kila fundi anamkosoa mwenzie unakuta umejenga nyumba ukamtumia fundi mmoja hadi kwenye lenta ukichukua mwingne cha kwanza anaanza kukosoa kazi ya mwenzie

Maana ya kumkosoa mwenzie ili umuone yeye anajua kuliko mwingine mwisho wa siku nayeye anatengeneza atakapoishia ukichukua mwingne anamkosoa alopita

Mafundi ni pasua kichwa sanah
Wamekaa kipigaji zaidi, akipata kazi anachowaza ni namna gani ampige boss kubwa.
 
Vitu kama hivi lazima uweke, kati ya bati na ukuta. Wengi wanachimbia tu bati linaingizwa kwa ndani, anasema cement kali inatosha, anachanganya na waterproof akidhani inatosha. Lazima uchezee dimbwi la maji ndani
View attachment 2806157
Fundi maiko hapo atakwambia usijali hilo niachie mimi kila kitu kitaenda sawa. Kuna ulazima gani wa kukubali kufanya kazi ambayo fundi anajua kabisa hawezi na ataiharibu
 
Huu uzi ni kama umenilenga mimi,lakini kwa kua ulikua ujenzi wangu wa Kwanza sijilaumu nimejifunza.

Lakini Kamwe sitojenga Dream House nifanye Hidden Roof, ukweli ni heri umwage Slab huko juuu kama wewe shida ni hutaki kuona BATI.

Lakini kujenga hidden roof tusidanganyane hizi nyumba za hivi si za kuishi mwanadamu ni special kwa wanyama wafugwao.

Aseee nimefumua Gypsum zote kwasababu zimeloa zimeshuka chini, hii hasara sitoisahau ila nimekoma na sirudiiii.

Hata uje uniambie wewe ni fundi uliebobea umesomea chuo bora duniani cha ufundi, Hunishawishi kuhusu Hidden Roof nikakuelewa.
Pole saña
 
Injinia umefunguka vyema kabisa, hapo kwenye Note fafanua zaidi kuna kitu kama nimeelewa hivi alafu kama sijaelewa.
Swali, hivi huwezi kumuwajibisha fundi kwa ishu kama hii?
NIlimaanisha kuwa contemporary unapoijenga hakikisha una mshauri kuanzia mwanzo na usitenganishe ulete fundi wa kujenga boma then baadae utafute wa roofing.

Hakikisha una msimamizi wa nyimba yako kama mshauri atakayehakikisja mchoro unafuatishwa bila kukosewa:.

Note: si kila mchoraji ili mradi anachora aweza kuku-dizainia nyumba hizi.

Zinahitaji mchoraji profesheno....najua hutanielewa tena.
Nakosa lugha rahisi zaidi
 
Ni nyumba za kisasa lakini bado hatuna mafundi wazuri wa kuweza kuzifanya ziendane na hali zote, zimekuwa ni nyumba nzuri sana kipindi cha kiangazi, kipindi cha mvua nyingi ni majanga matupu zinavuja mno lakini bado watu wanajenga sana nyumba kwa mtindo huo ambao sio rafiki hasa kipindi cha mvua.

Kuna mwenye nyumba hapa kila ikinyesha mvua lazima umuone fundi kapanda juu ya bati(navyotype tayari kuna fundi juu ya bati) na wapangaji wake wanalalamika sana maji kuingia ndani na kulowanisha vitu. Kila akiendelea kujenga style ni hiyo hiyo lawama nyingi akiziangushia kwa mafundi wake.

Mafundi upi ushauri wenu juu ya hili?
Upi ni mtindo mzuri wa kupaua nyumba kwa mazingira ya huku kwetu na aina ya mafundi tulionao mitaani?
View attachment 2805821
Hizo sio nyumba za maskini,kama una kipato Cha kuunga unga usiende huko.
 
Back
Top Bottom