Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kinaingia kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba, 2025 kikijivunia utendaji kazi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Kimesema kuwa kazi kubwa ya utelekezaji wa Ilani ya CCM, ikiwemo ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati ambayo kwa sasa imeiweka Tanzania kwenye ramani ya ushawishi mkubwa barani Afrika na ulimwenguni kwa ujumla.
Hayo yameelezwa jana jioni Machi 31, 2025 na Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Ndele Mwaselela akisema Rais Samia, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa na mgombea urais wa chama hicho, ni mwalimu wa vitendo miongoni mwa viongozi Afrika.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Amesema katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake, Rais Samia amegusa kila eneo katika maendeleo na kwamba, hawana sababu ya kuangalia wagombea wa vyama vingine ambavyo hawana rekodi za kufanya maendeleo.
"Tunaingia kwenye uchaguzi tukiwa tuna kiongozi na mwalimu wa maendeleo ya vitendo Afrika, hatuna sababu kuangalia hao wenzetu wataleta wagombea gani kwa kuwa, kazi iliyofanywa na mgombea wetu, hatuna shaka na ushindi wetu," amesema Mwaselela ambaye yuko kwenye msafara wa Wasira aliyekuwa ziarani Kanda ya Ziwa kuzungumza na wanachama na kukagua Ilani ya CCM.