Mjumbe wa Halmashauri kuu Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa kutoka Mkoa wa Mbeya Ndele Mwaselela amesema Rais wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuleta na kukuza vipaji vya viongozi vijana ndani ya Chama na Serikali.
Akizungumza kuhusu nafasi ya vijana katika uongozi ,Mwaselela amesema kuwa woga ni chanzo cha kushindwa kwa vijana wengi akitoa mfano wa ushindi wake kwenye nafasi ya ujumbe wa Halmashauri kuu ya( CCM) Taifa kupitia Mkoa wa Mbeya ,licha ya ushindani mkubwa kutoka kwa wagombea wenzie wanne.