Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Salaam Wakuu,
Nianze kuwatwanga maswali, hivi, enzi zenu ninyi wazee mlipokuwa mnatumia boon kusaidia familia zenu nani aliwaingilia huko? Mlipokuwa mnatumia boom kuwalipia wadogo zenu ada na kuwasaidia pesa za kujimu ili nao waweze pata elimu kama wewe kuna aliyewaingilia kwenye matumizi yenu?
Pia soma kauli nyingine za wabunge kuhusu boom:
Mkopo wenyewe unatolewa kwa dhulma, wengi wanaostahili wanapata 40%, 20% na wengine wanakosa kabisa.
Tukumbuke Boom ni pesa ya kujimu, ambayo ni kwaajilinya chakula na matumizi mengine madogo madogo ya mwanafunzi.
Hili Boom ndio linawasaidia baadhi ya wanafunzi kukamilisha sehemu ya ada ambayo mkopo haukukamilisha, kutokana na uzembe wenu mnaofanya wa kugawa mikopo kwa kujuana. Yaani serikalini kila sehemu ni upigaji, kia sehemu ni wizi na rushwa.
Baada ya kupiga kilele na kushupaza mishipa kuhakikisja kila mwanafunzi anayestahili anapata mkopo 100%, au wasome bure kabisa mnakuja kuongelea mambo ya kipuuzi. Hata wanafunzi wanao wanastahili kupumzika na kupumzisha akili zao, haimaanishi wao ni mashine 24/7 wapo na vitabu tu.
Embu tupunguzieni wadau kutokwa na mapovu mfanye mambo ya maana huko bungeni.
Tunawalipa mishahara minono na posho juu halafu mnaenda kufanya ujinga tu. Shame on you.
Posho zenu na mishahara inaishia kuwalipa machawa na watu wa kuwasafisha mitandaoni (Lucas Mwashambwa nakusalimu Mkuu) mmeona wananchi tukiwapigia kelele juu ya matumizi yenu? Kwanza zipunguzwe tu, mnatutia hasara tu walipa kodi, hatuoni faida ya uwekezaji wetu!

- Getere: Boom lifutwe, wanafunzi wanatumia kulewea
- Mbunge Jesca Mtambasavangu: Wanafunzi wanatumia Boom Kubeti badala ya Kusoma. Serikali itafute utaratibu mpya wa kuwakopesha