Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,752
- 7,861
View attachment 4152
...hii imekaaje? hawana wivu hawa?
...Kwa kawaida, Wamasai wana ndoa za mitala, hiyo ilifanywa ili kufidia idadi ya waliokufa kati ya watoto na morani kutokana na mfumo wa maisha yao. Mwanamke si wa mumewe tu, isipokuwa wa wanaume wote wa rika lake, mara nyingi ilitarajiwa kwa Mmasai anapotembelewa na mgeni anayelingana naye kwa rika, humkirimu kwa kumpa mmoja kati ya wake zake alale naye usiku. Lakini pia ni hiyari ya mwanamke mwenyewe kama anakubali kulala na yule mgeni au la. Kama akilala naye na kushika ujauzito, mtoto atakayezaliwa ni wa yule mume aliyemkaribisha mgeni na huhesabiwa katika ukoo wake katika mfumo wao wa kijamii. Kitala (talaka), huweza kutolewa kwa mke kukimbilia kwa baba yake, mathalan kutokana na kuteswa na mumewe. Kurejesheana malipo ya mahari, kuamua juu ya umiliki wa watoto baada ya tukio hilo, hufanywa kwa majadiliano yenye maelewano.
chanzo; Makala -Wamaasai (3) - Mgeni hukaribishwa mke alale naye
...hii imekaaje? hawana wivu hawa?