Mnh? Umasaini tena...!

Mnh? Umasaini tena...!

Mbu

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2007
Posts
12,752
Reaction score
7,861
View attachment 4152

...Kwa kawaida, Wamasai wana ndoa za mitala, hiyo ilifanywa ili kufidia idadi ya waliokufa kati ya watoto na morani kutokana na mfumo wa maisha yao. Mwanamke si wa mumewe tu, isipokuwa wa wanaume wote wa rika lake, mara nyingi ilitarajiwa kwa Mmasai anapotembelewa na mgeni anayelingana naye kwa rika, humkirimu kwa kumpa mmoja kati ya wake zake alale naye usiku. Lakini pia ni hiyari ya mwanamke mwenyewe kama anakubali kulala na yule mgeni au la. Kama akilala naye na kushika ujauzito, mtoto atakayezaliwa ni wa yule mume aliyemkaribisha mgeni na huhesabiwa katika ukoo wake katika mfumo wao wa kijamii. ‘Kitala’ (talaka), huweza kutolewa kwa mke kukimbilia kwa baba yake, mathalan kutokana na kuteswa na mumewe. Kurejesheana malipo ya mahari, kuamua juu ya umiliki wa watoto baada ya tukio hilo, hufanywa kwa majadiliano yenye maelewano.

chanzo; Makala -Wamaasai (3) - Mgeni hukaribishwa mke alale naye

...hii imekaaje? hawana wivu hawa?
 
Aise hii mwisho. Hivyo hata Mmachinga akienda kumtembelea rafiki yake wa Kimasai huachiwa kitanda na mke? Naomba wanaojuwa wanijuze.
 
wenye ufahamu mtujuvywe makabila mengine yenye mila na desturi ambazo 'si za kawaida' kwenye mahusiano ya mke na mume wa kimjini.
 
Wahaya nao nasikia wanatabia ya baba mkwe kulala na mkwewe wa kike. Hii laana kweli kweli.
 
Wahaya nao nasikia wanatabia ya baba mkwe kulala na mkwewe wa kike. Hii laana kweli kweli.

...ni katika mahusiano na mapenzi tu hayo pretty 🙂
 
kwa wamasai bora mlienda jandoni pamoja... yaani mko katika same age group.. your wife belongs to the entire age group, anayefika mbele anaweka mkuki nje ya hivyo vijumba vyao... mwenye nyumba akifika anakuta duh!!! kuna mwengine... ila is it really happening these days.... i know ni baadhi ya mila zinazopigwa vita katika fight against HIV/AIDS...

kwa wajaluo nao.. wife inheritance ipo... ukifariki kakako namridhi mkeo in the entire sense
 
Napenda kumshukuru mwandishi kwa uchambuzi wake kuhusu mila za jamii za kitanzania. Ila ningependa nitoe dosari chache tu katika uchambuzi huu kama ifuatavyo:
1. Kichwa cha habari kinapotosha kwa kiasi kikubwa kuhusu desturi aliyolenga kuzungumzia mwandishi. Kwa kawaida, kimila umasaini, mgeni hakaribishwi mke alale naye, bali, Mgeni hukaribishwa na hulala kwa mke. Lengo na nia siyo mgeni kulala na mke, ila ni ahifadhiwe kwa mke.

2. Binti ambaye bado hajafanyiwa tohara hawezi kamwe kuolewa hivyo swala la mahari ndogo halipo. Binti hufanyiwa tohara kwanza ndiyo apate kuolewa.

3. Ni makosa kwa mvulana ambaye hajafanyiwa tohara kuwa na mahusiano kumamiiana na binti ambaye hajafanyiwa tohara (mbaya zaidi kwa yule aliyefanyiwa tohara)kwa sababu mabinti wote ni wa morani.

Namwomba mwandishi azingatie maswala hayo matatu ili asiipotoshe jamii.
 
Aise hii mwisho. Hivyo hata Mmachinga akienda kumtembelea rafiki yake wa Kimasai huachiwa kitanda na mke? Naomba wanaojuwa wanijuze.

Lakini kabla hujaenda kumtembelea kwa tamaa hiyo bora ujue na yeye siku ajika kukutembelea usije ukawa mkali pengine kimila itabidi umuonyeshe uungwana.
 
Wahaya nao nasikia wanatabia ya baba mkwe kulala na mkwewe wa kike. Hii laana kweli kweli.

haipo hio kitu....umefananisha na wachaga

Sikutilia maanani nilipoona bandiko lako hapo kabla,
nimejaribu ku zoom zijalipata vizuri...

.....kuna bus moja la Saibaba la saa 6 mchana dar-arusha wanapanda sana wafanyabiashara wa kichaga hawa wanapenda speed kali ati wanakimbiza pesa.....

Haya madai ya Yo YO, kuna mwingine amewahi kusikia?

.
 
kwa wamasai bora mlienda jandoni pamoja... yaani mko katika same age group.. your wife belongs to the entire age group, anayefika mbele anaweka mkuki nje ya hivyo vijumba vyao... mwenye nyumba akifika anakuta duh!!! kuna mwengine... ila is it really happening these days.... i know ni baadhi ya mila zinazopigwa vita katika fight against HIV/AIDS...

kwa wajaluo nao.. wife inheritance ipo... ukifariki kakako namridhi mkeo in the entire sense

Nasikia unaweza kuweka mkuki kwa mwenzio ikiwa wewe na yeye ni best friends. Na u-best huo ni pale mnapokuwa mmekubaliana (mnakula mma/yamini or kind of).
 
Kuna jirani yangu kaoa Mbena wa Njombe kwenye safari zake kuna jioni alipita kijijini kwa bibi mzaa mama mkwe.Bibi akamwambia umechoka na safari kwanini usilale hapa na kuendelea na safari kesho asubuhi.Kukawa na msichana wa ukoo ule ambaye alimuhudumia maji ya kuoga,chakula na baadaye kumuonyesha pa kulala.Kasheshe ilikuwa usiku kama saa 4 yule msichana akaja chumbani na kanga 1 kumwambia jamaa mi ni mkeo usiku huu bibi kasema kwakuwa umeoa ukoo wetu.Jirani akaona hamna haja ya kuharibu mila akamkaribisha kitandani.
 
...duuuh! te -he -he -he!!! 😀 mila safi sana hiyo...au?
 
...duuuh! te -he -he -he!!! 😀 mila safi sana hiyo...au?

Hizi ni mila zenye kuleta madhara hasa wakati huu wenye UKIMWI.
Je ni mila kama hizi zilizokuwa zinatumika na baadhi ya watu kutafutia wageni wao wanawake - hasa wanapokuwa safari za kikazi?
 
Leo ndio nimetambua kuwa Mkuu "YO YO" ni "WAITU"
 
Hizi ni mila zenye kuleta madhara hasa wakati huu wenye UKIMWI.
Je ni mila kama hizi zilizokuwa zinatumika na baadhi ya watu kutafutia wageni wao wanawake - hasa wanapokuwa safari za kikazi?

Kuna habari niliwahi kusikia kwamba mwishoni mwa miaka ya 60's Nyerere alienda Kigoma usiku baada ya chakula Mkuu wa Mkoa akamuuliza Mwalimu kama atahitaji binti wa kumliwaza,naskia Mwalimu alikasirika na kushindwa kuongea kwa muda akamuuliza RC wakubwa wote wanaokuja mnawaletea? RC akajibu ndio,wengine hawangoji kuulizwa wanaomba wenyewe.
 
Makubwa!
Hizi stories ni nyingi - kuanzia za walimu wanaowapeleka wanafunzi wao kwa maofisa toka mawizarani mpaka majeshini ( JKT) zinapofanyika sherehe za maofisa, matron huchaguwa wale wasichana warembo wakaburudishe wageni.
Ukiangalia kwa undani huu wote ni unyanyasaji kwakisingizio cha takrima!- RUSHWA TU HII.
 
Back
Top Bottom