Mnielimishe: Ni kitu gani haswa Nyerere alikitaka kwenye Muungano, maana nachoona tunapigwa wazi wazi

Umeshawahi kujiuliza impact ya wazanzibari wooote kuhamia Bara au Wabara wooote kuhamia Zanzibar?
 
Mtanganyika atakodisha ardhi Zanzibar lakini Mzanzibari atamiliki ardhi Tanganyuka.
Sasa Zanzibar inakuwa ya wazanzibari tu wakati bara inakuwa na mchanganyiko.
Kwa nini? Kwaini kizazi cha zanzibar kinakuwa retained kihivyo wakati nchi ni moja.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Kama ardhi kule ndogo wahamie huku na wawauzie wabara wenye mitaji wawekeze kule kwa nini wabara wakose fursa kule wakati wao wanafursa huku.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
kwa Zaidi ya miaka50 na nyie mliwa pigaa kiwazi wazi, sasa ni zamu na wao ni zamu yao
 
Nadhani Tukitengana tutapoteza sehemu kubwa ya eneo la bahari na zanzibar itapaa kiuchumi kupitia marafiki zao waarabu.

In short kujitenga kuna manufaa makubwa sana kwa Zanzibar kukiko Tanganyika.
Zanzibar itapataje sehemu kubwa ya bahari wakati kuanzia tanga mpaka mtwara ni km ngapi za coast line ya Tanganyika. Pia umesahau kuna ukingo pia pale mafia island hawana uwezo wa kuendelea kumiliki chini ya mafia ktk ya mafia na znz ni nusu kwa nusu
 
Mkuu, nikuhakikishie, hili busu la Tanganyika na Zanzibar halitenguliwi ng'o; pamoja na huo unaousema nchi changa.
Jiografia hii iliyopo kati ya Tanganyika na Zanzibar huwezi kuifumbia macho. Hiyo historia ya waarabu haiwezi kuja huku kuondoa uhakika wa visiwa hivyo kuwa sehemu ya bara.
Waarabu walipokuja hawakutuuliza mahusiano kati yetu tokea enzi na enzi, kwa nini historia hiyo iwe pingamizi la uhusiano wa jadi?
 
Mipaka ya kizungu hii ndiyo tatizo! lkn kabla znz vilikuwa visiwa vya wavuvi tu! kutokea Rukwa, na bara kiujumla! sijui nani kawaroga nyie watu! mzungu? kifupi Bara Africa lilkuwa la wabantu loote hili mpaka mashariki ya kati! lilikuwa ni nchi mbili tu yaani Ethiopia na Misri tu!

sasa leo mzungu kawagawa mnanunian! acheni uchoyo! kesho utasema madaktari wooote ni wachaga tu! tugawane sawa! '' wewe na uzee wooote huu si mlikuwa mnaimba binadam wote sawa na africa ni moja? siyo nyie!! ndo mnaanzaga hivi!! fanya kazi bwege weee!

tena wazanzibar tunawaajili zaidi na zaidi!! wale mpaka wasaze!! wacha walime na asiwaguse mtu! ole wako!! uvivu tu! Weye una shamba wapi? mi bara yooote hii tukiamua kulima tutapanda na kuvuna kila kona ya nchi, tutaomba na ardhi nje! tena siyo hao tu Kenya rwanda, burundi,uganda,zambia malawi, msumbiji, SA,nk wanakuja liaaaa! pasuka! tukuzike..... Africa one
 
Mipaka ya kizungu hii ndiyo tatizo! lkn kabla znz vilikuwa visiwa vya wavuvi tu! kutokea Rukwa, na bara kiujumla! sijui nani kawaroga nyie watu! mzungu? kifupi Bara Africa lilkuwa la wabantu loote hili mpaka mashariki ya kati! lilikuwa ni nchi mbili tu yaani Ethiopia na Misri tu!

sasa leo mzungu kawagawa mnanunian! acheni uchoyo! kesho utasema madaktari wooote ni wachaga tu! tugawane sawa! '' wewe na uzee wooote huu si mlikuwa mnaimba binadam wote sawa na africa ni moja? siyo nyie!! ndo mnaanzaga hivi!! fanya kazi bwege weee!

tena wazanzibar tunawaajili zaidi na zaidi!! wale mpaka wasaze!! wacha walime na asiwaguse mtu! ole wako!! uvivu tu! Weye una shamba wapi? mi bara yooote hii tukiamua kulima tutapanda na kuvuna kila kona ya nchi, tutaomba na ardhi nje! tena siyo hao tu Kenya rwanda, burundi,uganda,zambia malawi, msumbiji, SA,nk wanakuja liaaaa! pasuka! tukuzike..... Africa one
 
zanzgar tu!! yaani mayote madagascar usheli sheli tuna vitaka pia! bi mali yetu!
 
Jiografia mbona ipo pia baina ya Tanzania na nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi lakini hakuna muungano? Kwa nini Muungano wa Zanzibar ndiyo muhimu zaidi?
 
Naombeni wenye jicho la ziada mnitoe ujinga maana huu ujinga nilionao ndio unanifanya niwe napatwa na hasira kwa maono mafupi yanayonifanga nione Zanzibar inatunyonya
Mkuu Mwanajeshi wa Angani, sky soldier , kwanza asante kujikubali wewe ni mjinga, kutokana na maono mafupi kuwa Zanzibar inatunyonya, hivyo kupatwa na hasira. Uzuri wa kujikubali ujinga, ni ukielimishwa, ujinga utakutoka, hivyo karibu hili darsa langu.
Si mara moja wala mbili, niliwahi kusisitiza humu, Watanzania waelimishwe historia ya muungano, chanzo halisi ni nini na ni nani. Japo ni kweli waasisi wa muungano wetu huu adhimu ni Nyerere na Karume, lakini kuna chanzo, sababu, na mtu aliyemuanza mwenzake kutaka muungano. Kwanza futa hiyo kauli kuwa Nyerere "alimbembeleza sana Karume kuwe na muungano", ni kauli ya kijinga tuu kwa kutokujua, hivyo Wazanzibari wengi na wasioutakia mema muungano wetu kudhani chanzo ni Nyerere!.
Chonzo Halisi cha Muungano ni Karume, Nyerere Akamalizia!.
Baada ya yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, yaliyomng'oa Sultani, Sultani alikimbilia Uingereza, na kuomba msaada, zikatumwa meli vita kuja kuadabisha Zanzibar ili kumrejesha Sultani. Karume ndio akavuka maji, kuja Bara, kumuomba Nyerere ulinzi ili Tanganyika iliilinde Zanzibar dhidi ya kipigo cha Mungereza kinachofuata na kumrejesha Sultani!.
Sasa katika kuwaza na kuwazua Tanganyika itaisaidia kuilinda vipi Zanzibar dhidi ya Uingereza?, ndipo Mwalimu akatoa wazo, "tuungane". Karume akakubali hapo hapo na kusema "Tuungane hata leo, wewe rais, mimi makamu". Karume alidhamiria muungano wa nchi moja na alitaka utangazwe kesho yake!. Ni Nyerere alimkatalia, kutokana na Tanganyika kuwa ni li nchi likubwa, tukiungano kuwa nchi moja, itaonekana Tanganyika imeimeza Zanzibar, hivyo ni Nyerere ndio alimkatalia Karume muungano wa nchi moja na kuipatia Zanzibar status ya "the minority" kwenye muungano huu. Hivyo chanzo cha muungano ni Zanzibar, alitaka ulinzi, aliyemuanza mwenzie ni Karume, Nyerere alimalizia!.
Miungano yote duniani ni kama ndoa, kuna give and take, na siku zote kwenye muungano wa the majority na minority, siku zote the minority ndio anafaudu. Zanzibar ni the minority. Ndani ya structure hii ya muungano, Tanzania ni nchi moja, ndani ya nchi moja hii kuna uraia mmoja tuu, uraia wa Tanzania, hivyo kila Mtanzania ni Mtanzania tuu, hakuna Mtanzania Bara wala Mzanzibari, kuna raia mmoja tuu , Mtanzania, hivyo Wazanzibari wote wana haki zote za Utanzania swa na Mtanzania mwingine yoyote ikiwemo kumiliki ardhi, ajira, uongozi na kila kitu, yaani kila Mzanzibari ni Mtanzania mwenye haki zote.

Lakini ndani ya the majority ya Utanzania, kuna the minority ya Uzanzibari, ambao ni special kwajili ya Wazanzibari pekee, hivyo kila Mzanzibari, kwanza ni Mtanzania, kisha ni Mzanzibari, lakini sio kila Mtanzania ni Mzanzibari, Mtanzania ni Mtanzania tuu Wazanzibari wakiwemo, ila Mzanzibari ni Mtanzania ambaye pia ni Mzanzibari, an added advantage!.
haya malalamiko kutoka Zanzibar kwamba wananyonywa yaliwekwa kimkakati ili iwe silaha kwa wazanzibar kuridhika na kujitapa kwamba wametuzidi akili, ingekuwa hivi muungano ungekufa mapema.
Hao Wanzanzibari wanaolalamika wananyonywa nao ni wajinga tuu kama Watania wanaolalamika wananyonywa. Muungano wetu ni wa milele!. Hauwezi kufa kwasabu tutaulinda kwa gharama yoyote.
lakini pia haya malalamiko yapo kimkakti kuizubaza Tanganyika idhani kwamba Zanzibar ni kama mkoa wake kumbe kiukweli wazanziba ndio wanaonufaika.
Hii pia sii kweli, kwenye muungano wote tunanufaika, ila pia ni ukweli usiopingingika the minority anafaudu zaidi!.

Mwisho.
Muungano kama ndoa!.
Hili naomba nisilifafanue lisije likawatia watu hasira, ila siku hizi kuna wanaume wa ajabu, mtu anaoa mke, ana jukumu la kumhudumia, lakini anamuonea wivu eti mke anafaidi kula bure, kulala bure, lakini anasahau zile huduma ambazo zinalipiwa na kugharimikiwa. Ndani ya ndoa nani anafaidi zaidi au kufaudu zaidi?.
P
 
Kwanza kabisa nimeona ramani na hutwo Tu dot tuwili nikacheka. Hivi ndo hutwo tunashare kweli kwamba tuliungana?

Pili ,sikujua kama ajira Wana apply kama Sisi nikajua zipo nsfasi maalum kama uhamiaji NK

Tatu , ukikutana na mzanzibar yeyoye ni mwendo kubweka kuwa hawautaki muungamo huko wakitunyonya.

Nne hivi hao vichwa vinavuoangalia Kero vya upande wetu havioni kuwa hiyo ni Kero ? Huku wanajitapa wanataka Zanzibar Kamili ? Huu ni uzwazwa
 
Nami nimefaidi .binafsi sijawahi kumsikia mzanzibar akijitambulisha kama mtanzania sijui hii imekaaje. Pili unadhani muungano ukifa mwarabu anaweza kurudi? Una habari huyo mwarabu alokimbilia uingereza kwamba bado anajipa hadhi ya kuwa mtawala wa Zanzibar ?

Mwisho juzi nimemsikiliza jusa anadai mwingereza alimsaidia kambarage kuitawala Zanzibar nawe unasema sultani angesaidiwa na mwingereza .tuelewe lipi Mzee Baba
 
Tatizo nyie vijan hamuelewi, Nyerere aliona mbali sana for security reasons kwasababu hata leo hii zanzbar wakijitenga hawata survive coz watakua week kijeshi kitendo cha nyerere kuleta muungano ni kutaka ku access eneo kubwa la bahari ya hind
Huu ujinga mim ndo staki Et security reason , Hao wazanzibar ndo wanatulinda Kuna Kilomita 200 za bahari za kwetu baharini , hata Kama US, China, Russia akitaka kutupiga anashindwa, anaweza kutupiga hata akiwa kwo inshort Muungano ni Nonsense kabisa siku nikiwa raisi ni serikali Tatu au kuvunja Muungano basi
 
Za ndan ndan znasema et mpaka halis wa zenji ni kuanzia chalinze kuja dar kwenda had zenj..so wakisema wanavunja muungano unaambiwa dar na mkoa wa pwan wote wao....ndomana haitakiw hata kutamka
 
Katiba Mpya ingeweka serikali 3 na usawa mzuri katika muungano. Kuna mambo mengi hayako sawa kama mtoa mada alivyoeleza. Watu wa Zanzibar wana upendeleo sana katika huu muungano.

Katiba Mpya ya serikali 3, ingefuta haya matatizo ya muungano kabisa.
 
Hio siku ikifika utakuwa ushakufa zamani sana, ni miaka 2000 ijayo, ila kama kweli upo serious unataka kuishuhudia basi anza ule ubaguzi wa kiafrika Kusini dhidi ya wapemba na waunguja , anza Harakati za kuwatimua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…