Mnyama Airport Kwenye Runway: Marubani Wapewa Tuzo

Mnyama Airport Kwenye Runway: Marubani Wapewa Tuzo

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Nimesoma habari hii:

Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi nchini Tanzania, imesema itawazawadia tuzo maalumu Rubani Suhad Soud Kassim na Ofisa Daraja la kwanza, Alessandro Morgan kutokana na ujasiri walioonesha na kufanikiwa kuzuia kutokea ajali ya ndege.

Marubani hao ni wa Shirika la Ndege (ATCL), imeeleza kuwa walionesha ujasiri kwa kuzuia kutokea ya ajali ya ndege yao yenye namba TC 110 Airbus A 220 ikiwa na abiria 84.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Gabriel Migire ameahidi hayo, wakati akifungua kikao cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa ATCL, lililofanyika Machi 30, 2022 mjini Morogoro

“Wizara pia itafanya jambo kwa kutambua mchango mkubwa uliofanywa na marubani hao , siyo kwa maana ya kupendelea na siyo kwa maana wengine hawakufanya vizuri, lakini walifanya jambo la ajabu sana.Walifanya maamuzi magumu ambayo kwa kweli yanapaswa kutambuliwa na serikali na wadau wengine,” amesema Katibu Mkuu.

Kwa mujibu wa Uongozi wa ATCL, marubani wa ndege hiyo iliyokuwa ikiruka jioni ya Septemba 29, 2020, Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro ( KIA) kuelekea Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, ikiwa kwenye kasi kujiandaa kuruka marubani hao walimuona mnyama kwenye njia ya kurukia.

Uongozi wa ATCL umeeleza kwamba marubani hao walitumia ujasiri wa kuisimamisha ndege hiyo, ili isifikie kumgonga mnyama huyo kwenye hatua ya kupaa angani, jambo lililoteta taharuki kubwa kwa abiria, ndugu na taasisi kwa ujumla.

Inakuwaje airport haina ulinzi wa kutosha hadi kuacha wanyama kujitembelea kwenye runway? Ina maana hata gaidi anaweza kuingia kwenye boarding area kutokea huko vichochoroni na kuteka ndege.
 
Hilo swala waliloongea hapo Ni Ngumu sana kufanyika kama Ni kweli wapewe pongezi hasa! Wakati nikiendelea kujiuliza hiyo ndege kama Ilishafikia Take-Off Distance....Hapo lazima yangekua majanga.
 
Hatuwezi kuamini hadisi zisizokuwa specific. Wataje jina la mnyama. Watuambie baada ya uchunguzi wamegundua nini kuhusu usalama wa kiwanja husika.

Lakini wasije wakatuambia atakuwa paka alipelekwa kichawi. Wengine uchawi tunausikia tu lakini hatuamini kwa asilimia zote.
 
pale kia kuna punda sana,,wachina wamenunua sana punda ili masai wanunue pikipik zao lakin punda hawaishi,,tahadhari sana hasa ukiwa highway ya moshi-arusha pale mijohoroni kuna punda kama laki hivi kila siku wanagongwa..tena ukute ni IST au Vangad inaisha yote unauza skrepa.punda mgumu kuliko mti
 
Yaani ndege imeshika kasi na kila utaratibu umefanyika information zote zimeingizwa kwenye mfumo Mara ghafla mnyama akakatiza wakashika break na kurudi reverse kuanza tena au sio.
Ndege ya kawaida ya abiria inarudi reverse haya ni maajabu ya karne.
Labda ivutwe ....
 
pongezi kubwa kwa hao marubani nilijua kuwa marubani majasiri ni wale waliotoka jeshini tu kumbe wapo raia majasiri vilevile
 
pale kia kuna punda sana,,wachina wamenunua sana punda ili masai wanunue pikipik zao lakin punda hawaishi,,tahadhari sana hasa ukiwa highway ya moshi-arusha pale mijohoroni kuna punda kama laki hivi kila siku wanagongwa..tena ukute ni IST au Vangad inaisha yote unauza skrepa.punda mgumu kuliko mti
Mkuu umeongea kweli..punda ni mnyama mgumu sana
 
pale kia kuna punda sana,,wachina wamenunua sana punda ili masai wanunue pikipik zao lakin punda hawaishi,,tahadhari sana hasa ukiwa highway ya moshi-arusha pale mijohoroni kuna punda kama laki hivi kila siku wanagongwa..tena ukute ni IST au Vangad inaisha yote unauza skrepa.punda mgumu kuliko mti
Uwanja umezungushiwa fence kuanzia mbele,njia ya kwenda mererani,nyuma yake kijiji cha majengo sasa huyo mnyama kapita wapi au ni sungura
 
Uwanja umezungushiwa fence kuanzia mbele,njia ya kwenda mererani,nyuma yake kijiji cha majengo sasa huyo mnyama kapita wapi au ni sungura
mara elfu 50 uwanja wa arusha kisongo una quality,,ingawa ni local..
kia ni international airport lakini nakwambia iko siku ndege itakwama kwenye matope pale na abiria watashuka na kuisukuma!!unashangaa punda kuingia!!
 
Mfumo wa ndege ni automatic sasa iliwezaje kurafrain wakati mfumo wote umeshakubali taarifa na ukaruhusu take off au ni ndege mnana?
 
Yaani ndege imeshika kasi na kila utaratibu umefanyika information zote zimeingizwa kwenye mfumo Mara ghafla mnyama akakatiza wakashika break na kurudi reverse kuanza tena au sio.

Mfumo wa ndege ni automatic sasa iliwezaje kurafrain wakati mfumo wote umeshakubali taarifa na ukaruhusu take off au ni ndege mnana?
Kama speed ya ndege ilikuwa haijafikia V1 itasimama tu rubani akiiweka kwenye reverse thrust, isipokuwa stopping distance haiwezi kuwa kama hiyo ya baiskeli wanayosema. Kuna accident ilitokea Tenerife huko visiswa vya Canary mwaka 1977 baada ya pilot wa KLM kushindwa kusimama ghafla kwa vile tayari ndege ilishazidi hiyo sipidi ya V1. Tatizo ni kwamba haiwezekani uwanja uruhusu watu na wanyama kutembea hovyo. Matatizo ambayo huwasumbua mapailot ni ndege kuingia kwenye injini, laksi siyo ya mnyama kukatisha uwanjani

Hii ni kweli au ni mafumbo ya CCM na maamuzi yake?
 
Moja kati ya majukumu muhimu na la kwanza kwa operations officer ni kufanya airfield inspections on maneuvering areas (runways &taxiways) mda mchache kabla ndege haijatake off au kuland. kama angetimiza majukumu yake yote hayo yasingetokea. Mfano kobe mara nyingi ndo utawakuta wengi katikati ya runways hasa kipind cha mvua nyingi na huweza kusababisha hasara sana
 
Back
Top Bottom