Mnyama Airport Kwenye Runway: Marubani Wapewa Tuzo

Mnyama Airport Kwenye Runway: Marubani Wapewa Tuzo

Nimesoma habari hii:

Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi nchini Tanzania, imesema itawazawadia tuzo maalumu Rubani Suhad Soud Kassim na Ofisa Daraja la kwanza, Alessandro Morgan kutokana na ujasiri walioonesha na kufanikiwa kuzuia kutokea ajali ya ndege.

Marubani hao ni wa Shirika la Ndege (ATCL), imeeleza kuwa walionesha ujasiri kwa kuzuia kutokea ya ajali ya ndege yao yenye namba TC 110 Airbus A 220 ikiwa na abiria 84.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Gabriel Migire ameahidi hayo, wakati akifungua kikao cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa ATCL, lililofanyika Machi 30, 2022 mjini Morogoro

“Wizara pia itafanya jambo kwa kutambua mchango mkubwa uliofanywa na marubani hao , siyo kwa maana ya kupendelea na siyo kwa maana wengine hawakufanya vizuri, lakini walifanya jambo la ajabu sana.Walifanya maamuzi magumu ambayo kwa kweli yanapaswa kutambuliwa na serikali na wadau wengine,” amesema Katibu Mkuu.

Kwa mujibu wa Uongozi wa ATCL, marubani wa ndege hiyo iliyokuwa ikiruka jioni ya Septemba 29, 2020, Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro ( KIA) kuelekea Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, ikiwa kwenye kasi kujiandaa kuruka marubani hao walimuona mnyama kwenye njia ya kurukia.

Uongozi wa ATCL umeeleza kwamba marubani hao walitumia ujasiri wa kuisimamisha ndege hiyo, ili isifikie kumgonga mnyama huyo kwenye hatua ya kupaa angani, jambo lililoteta taharuki kubwa kwa abiria, ndugu na taasisi kwa ujumla.

Inakuwaje airport haina ulinzi wa kutosha hadi kuacha wanyama kujitembelea kwenye runway? Ina maana hata gaidi anaweza kuingia kwenye boarding area kutokea huko vichochoroni na kuteka ndege.
Hivi Golikipa akiokoa Michomo ambayo ndiyo sehemu ya Kazi yake awapo Golini anatakiwa Kusifiwa?

Leo mnawasifu hawa Marubani kwa Kupiga Break Kali na Kutomgonga huyo Mnyama je, ingeyokea wamesimama hivyo ghafla halafu Ndege ikalipuka na Wakafa pamoja na hao Abiria wao 84 bado mngekuja Kuwakongole ( Kuwasifia ) Kinafiki hivi?

Yaani GENTAMYCINE niwe Rubani tena wa Ndege Kubwa halafu nimebeba Abiria wa Kutosha nimeshaiseti Ndege tayari kwa Kupaa ( Kuruka ) kisha ajitokeze Mnyama au Mlevi Mmoja mbele yangu nipunguze mwenfo ili nimuokoe? Mimi nafyeka Mnyama na huyo Mtu kisha napaa zangu kutafuta Futi 55000 za Usawa wa Bahari kuitafuta JNIA.
 
Mzee wangu, mimi nimekopi yaliyotolewa na wenyewe, siyo kwamba ninawasifu kwani naona kamaumeniunganisha na kundi hilo. Tunategemea kila mtu kutekeleza wajibu unaoendana na majukumu yake, ila sasa kwetu sisi wabunge wakitekeleza wajibu wao, wanapewa posho; kwa hiyo inawezekan ndiyo ada yetu.
 
Nakumbuka baadhi ya abiria walitapika baada ya tukio ilo. Kuna wadada walikua jirani pale walihisi kukojoa kwa hofu.

Wale marubani wapewe uwaziri kabisa
 
Back
Top Bottom