Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, amethibitisha kuwa fedha zote zinazochangwa na wananchi pamoja na wanachama, ikiwemo mifumo ya kielektroniki na zile za "tonetone" zinazokusanywa mikutanoni, ziko salama kabla na baada ya matumizi.
Mnyika aliongeza kuwa, kwa mujibu wa taratibu za kifedha za kitaasisi, yeye kama Katibu Mkuu ndiye Afisa Masuhuli wa chama ambaye anasimamia uidhinishaji huo. Ili fedha ziweze kutoka kwenye akaunti za benki za makao makuu ya CHADEMA, kuna kategoria mbili za watia saini ambazo ni lazima zihusike kutoa idhini hiyo. Kategoria ya kwanza inajumuisha nafasi ya Mwenyekiti wa Chama na Katibu Mkuu, huku kategoria ya pili ikiwa na Mkurugenzi wa Fedha pamoja na maafisa wengine walioidhinishwa.
Tuhuma za matumizi ya pesa kwa viongozi ni uongo, pesa ziko salama