Mnyika: Bado Ofisi ya Msajili inatafuta njia Shughuli za CHADEMA zisimamishwe, tumeandikiwa barua tujieleze

Mnyika: Bado Ofisi ya Msajili inatafuta njia Shughuli za CHADEMA zisimamishwe, tumeandikiwa barua tujieleze

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Kutoka mahaka kuu kanda ya Dar esSalaam kesi ya maombi madogo namba 8960 ya Said Issa Mohammed dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema imepelekwa mbele mpaka Mei 20, mwaka huu.

Kesi hiyo iliitwa tena leo Mei 13, 2026 ambapo pande zote mbili kupitia mawakili wao zilitoa hoja zao ambazo zilisikilizwa ili kutolewa maamuzi na mahakama.

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika amesema licha ya Chama hicho kuondolewa kizuizi cha kutofanya shughuli zake bado Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inatafuta njia CHADEMA kusimamishwa tena akidai wamepewa barua ya kuwataka wajieleze.

Aidha Mnyika ameeleza kuwa hawezi kuweka hadharani ujumbe waliopewa kwenye barua hiyo kutoka kwa Msajili, akitoa wito kwa wananchi kuendelea kupigania haki

​
 
Nilisema kuhusu hili hapa siku si nyingi:

Kutoka mahaka kuu kanda ya Dar esSalaam kesi ya maombi madogo namba 8960 ya Said Issa Mohammed dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema imepelekwa mbele mpaka Mei 20, mwaka huu.

Kesi hiyo iliitwa tena leo Mei 13, 2026 ambapo pande zote mbili kupitia mawakili wao zilitoa hoja zao ambazo zilisikilizwa ili kutolewa maamuzi na mahakama.

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika amesema licha ya Chama hicho kuondolewa kizuizi cha kutofanya shughuli zake bado Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inatafuta njia CHADEMA kusimamishwa tena akidai wamepewa barua ya kuwataka wajieleze.
eeeh,
nendeni mkajieleze sasa au hamna maelezo mchukuliwe hatua zaidi za kisheria?
 
Hiuyo Msajili ni mteule wa nani?

Mwisho wenu opo tu.
Gentleman,
msajili ni muajiriwa mwenye dhamana ya umma, na anafanya kazi ya umma kwa kodi ya wananchi waliompatia dhamana hiyo.
huyo nii mteule wa waTanzania wote kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi.
 
eeeh,
nendeni mkajieleze sasa au hamna maelezo mchukuliwe hatua zaidi za kisheria?
Jibu jepesi sana,kama hawataki siasa za ushindani wafute mfumo wa vyama vingi mbaki pekee yenu.

Lakini ninyi wanaufaika wa mfumo,bila CHADEMA madhubuti kazi za kujitoa akili zitapotea,mtarudi kijiweni kwenye maisha ya mateso,piganieni mfumo uwatoe kwenye ukupe,Slogan ya Mwl ilikuwa usiwe kupe,Nini uchawa
 
usipo kua mtiifu na usie na adabu,
utatiishwa na kushikishwa adabu kwa lazima tena kwa mujibu wa sheria unazopuuza na kisha utambwembwela zaidi kwa mayowe nonsense yasiyokusaidia chaochote baadae.

umeambia nenda katoe maelezo,
ugumu uko wapi hao kwa mfano kama sio kiburi nonsense cha kuzaliwa?
 
Spana zinawaingia

Ova
sasa,
umeambiwa katoe maelezo, kistaarabu kabisa,
unashupaza shingo na kumbwelambwela mitandaoni kuatract public sympathy isiyo kusaidia, hiyo ni akili au matope gentleman?:pedroP:
 
Hakuna upinzani unaopangiwa,kazi hiyo wape wenzenu wa CHAUMMA na shikizi wenzao.

Simlitaka siasa ya vyama vingi kwanini mbinu chafu zinawaindolea umadhubuti wenu,au ndiyo siku za miaka 60 ya ustaafu zinavunja kabisa uwezo wa kufikiri.

Mzee Warioba ana miaka 86 kwanini na uzee wake anawazidi uwezo wa kufikiri wanachama 12M!

Ukiona taasisi Ina deal na mtu ujue imeshiwa pumzi inambwelambwela kama maiti iliyokuwa inakaribia kuachia roho
 
Back
Top Bottom