Mnyika: Bavicha ngazi zote kuanzia taifa hadi Msingi undeni kamati za kudai Katiba mpya kabla hatujaingia rasmi mitaani!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Katibu mkuu wa Chadema J J Mnyika amevitaka vikao vyote vya kikatiba vya Bavicha kuanzia Taifa hadi Msingi kuandaa kamati za kudai Katiba mpya.

Mnyika amesema ni vema wakajipanga sawasawa kabla ya kuingia rasmi mitaani kushinikiza uundwaji wa katiba mpya.

Nawasalimu kwa jina la JMT!
 
Hawa watu wanajaribu kupimana ubavu na rais,kuwa fair kwa vyama vya kihuni huni Kama chadema ni kuliangamiza taifa,

Rais Hana budi kubadili mikakati ya kudili na vyama vya kihuni huni Kama hivi ili kuliepusha taifa kuingia kwenye machafuko.

Walikuwa wapi kudai katiba enzi za JPM,why now ,je wamemuona rais ni mtu dhaifu kwao hivyo ni muda muafaka wa kuanzisha chokochoko?

Chadema nawahakikishia kile mnachokitafuta hakika mutakipata muda si mrefu,wait and see.
 
Wananchi tupo ila nyie viongozi muwe mstari wa mbele sisi wananchi tuwe nyuma yenu

Uko sahihi sana, hata wakati wa vita vya Uganda wananchi walikuwa tayari, je Nyerere alikuwa mstari wa mbele huko vitani? Hawa askari wote wanaokwenda kulinda amani sehemu zenye vita, viongozi wanaosaini hiyo mikataba na wao huwa wanaenda huko kwenye vita wao na familia zao? Kwenye mechi za soka huwa kunakuwa na kocha, je huwa naye anaingia uwanjani kucheza?

Hizi lugha za kijinga ndio hutengenezea uhalali wa viongozi kusigina haki na maslahi ya watu. Ndio maana unaona viongozi wanaoishi hapa Dar wanatembelea maVX ya 400m+, huku wao wakiwa na maji safi ya kuflash mpaka vinyesi, wakati huko vijijini watu wakosa hata kisima cha maji cha 50m tu. Na mleta post unaona umepost kitu cha maana kwelikweli.
 
Hawa watu wanajaribu kupimana ubavu na rais,kuwa fair kwa vyama vya kihuni huni Kama chadema ni kuliangamiza taifa,

Rais Hana budi kubadili mikakati ya kudili na vyama vya kihuni huni Kama hivi ili kuliepusha taifa kuingia kwenye machafuko.

Walikuwa wapi kudai katiba enzi za JPM,why now ,je wamemuona rais ni mtu dhaifu kwao hivyo ni muda muafaka wa kuanzisha chokochoko?

Chadema nawahakikishia kile mnachokitafuta hakika mutakipata muda si mrefu,wait and see.

Kwa taarifa yako hata rais mumjaze mtakavyo hata ikibidi kuifuta cdm, bado katiba mpya itapatikana. Hata angefufuka Magufuli leo hii bado katiba mpya ingepatikana. Na vile alikuwa ameshaangusha uchumi, tena yeye ingepatikana hata kwa machafuko. Hitaji la katiba mpya ni la wakati, halikwepeki kwa hila wala mabavu. Someni alama za nyakati.
 
Uko sahihi sana, hata wakati wa vita vya Uganda wananchi walikuwa tayari, je Nyerere alikuwa mstari wa mbele huko vitani? Hawa askari wote wanaokwenda kulinda amani sehemu zenye vita, viongozi wanaosaini hiyo mikataba na wao huwa wanaenda huko kwenye vita wao na familia zao? Kwenye mechi za soka huwa kunakuwa na kocha, je huwa naye anaingia uwanjani kucheza?

Hizi lugha za kijinga ndio hutengenezea uhalali wa viongozi kusigina haki na maslahi ya watu. Ndio maana unaona viongozi wanaoishi hapa Dar wanatembelea maVX ya 400m+, huku wao wakiwa na maji safi ya kuflash mpaka vinyesi, wakati huko vijijini watu wakosa hata kisima cha maji cha 50m tu. Na mleta post unaona umepost kitu cha maana kwelikweli.
Sawa nenda ukaandamane uvunjwe mguu huku viongozi wa chadema hawana muda na wewe.

Bogus lema alivotoka jela alikuja na nyimbo kuwaimbia watu kwenye viwanja vya samunge Arusha mjini sasa na ww ukivunjwa mguu wakati wazazi wako wanapambana hospitali viongozi wa chadema wanakutungia nyimbo
 
Kwanini Ma VX hupatikana haraka?
Kwanini maji huwa nimchakato 60yrs,mito,maziwa na mabwawa tunayo.
 
Mnyima bado hajapona ugonjwa wake, alazimishwe kurudi hospital
 
Yaa
Hawa watu wanajaribu kupimana ubavu na rais,kuwa fair kwa vyama vya kihuni huni Kama chadema ni kuliangamiza taifa,

Rais Hana budi kubadili mikakati ya kudili na vyama vya kihuni huni Kama hivi ili kuliepusha taifa kuingia kwenye machafuko.

Walikuwa wapi kudai katiba enzi za JPM,why now ,je wamemuona rais ni mtu dhaifu kwao hivyo ni muda muafaka wa kuanzisha chokochoko?

Chadema nawahakikishia kile mnachokitafuta hakika mutakipata muda si mrefu,wait and see.
Yaani kuwa na katiba mpya kwako ni kuliangamiza taifa au ulikiwa unaana kuiangamiza ccm ila umekosea tu!!
 
Wala hamjamuelewa Mnyika. Kuingia mitaani hakuna maana kuleta vurugu Wala kuandamana. Maana yake Ni kuanza kuwaeleza wananchi au kuwa ndo agenda yao huko mitaani.
 
Kuna tofauti kati ya kuingia mtaani na kuingia msituni.

Umeeleweka bwashee!
 
Uko sahihi sana, hata wakati wa vita vya Uganda wananchi walikuwa tayari, je Nyerere alikuwa mstari wa mbele huko vitani? Hawa askari wote wanaokwenda kulinda amani sehemu zenye vita, viongozi wanaosaini hiyo mikataba na wao huwa wanaenda huko kwenye vita wao na familia zao? Kwenye mechi za soka huwa kunakuwa na kocha, je huwa naye anaingia uwanjani kucheza?

Hizi lugha za kijinga ndio hutengenezea uhalali wa viongozi kusigina haki na maslahi ya watu. Ndio maana unaona viongozi wanaoishi hapa Dar wanatembelea maVX ya 400m+, huku wao wakiwa na maji safi ya kuflash mpaka vinyesi, wakati huko vijijini watu wakosa hata kisima cha maji cha 50m tu. Na mleta post unaona umepost kitu cha maana kwelikweli.
Mifano haiendani bwashee..
Kuweni front na famalia zenu.
 
Chama cha siasa kikishindwa uchaguzi mara 3 kinageuka kuwa cha kigaidi..

Ndiko hii saccos chadema inakoelekea
 
Mna mbadilisha huyu mama muda kidogo mtamuita DIKTETA ...
 
Wala hamjamuelewa Mnyika. Kuingia mitaani hakuna maana kuleta vurugu Wala kuandamana. Maana yake Ni kuanza kuwaeleza wananchi au kuwa ndo agenda yao huko mitaani.
Tunawakaribisha mtaani Boss leo kesho wao tu.
 
Back
Top Bottom