Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, amekanusha vikali madai kuwa Shilingi Milioni 900 zilizotolewa na wafadhili zitatumika kufadhili maandamano ya mwezi ujao, akisisitiza kuwa kauli hizo ni propaganda za uongo zinazosambazwa na kada wa CCM, Ally Hapi.
Mnyika ametoa ufafanuzi huo leo Jumatano, Juni 17, 2026, ambapo ameweka wazi kuwa fedha hizo zilisharudishwa kwa wafadhili tangu Desemba mwaka jana baada ya chama kuwekewa zuio haramu la utendaji la siku 309, na kwamba zilikuwa maalum kwa ajili ya mradi wa jinsia na mafunzo ya uongozi kwa wanawake.
"Ally Hapi analeta propaganda za uongo kujaribu kuhusisha fedha hizo na maandalizi ya maandamano. CHADEMA si chama kinachovunja mikataba au kutafuna pesa za wadau. Fedha hizo hazitatumika kwenye maandamano; zilikuwa za mradi wa wanawake na utaratibu wa kuzirudisha kwa nchi husika ulishafanyika baada ya mradi kufika ukomo tukiwa kwenye zuio," amesema Mnyika.
Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa msaada wa fedha za nje ndani ya CHADEMA haufiki hata asilimia 2 ya bajeti yote, na kuitaka CCM nayo iweke wazi mamilioni inayopata kutoka kwa taasisi na vyama marafiki vya nchi za Magharibi na Mashariki badala ya kushambulia upinzani.