Pre GE2025 Mnyika: Mapambano yamewezesha Faye kushinda Uchaguzi wa Rais Senegal, November 2023 nilikuwa Senegal kusaidia Harakati za Upinzani!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huku Tanzania wapinzani wamelamba asali hawana jipya tena
 
Katibu mkuu wa Chadema mh John Mnyika amesema Mapambano yamewezesha mh Faye kushinda Uchaguzi wa Rais Senegal

Mnyika anasema November 2023 alikuwa Nchini Senegal kama sehemu ya Ujumbe kutaka kiongozi wa Upinzani mh Sonko na mwenzake waachiwe Huru

Mnyika ameeleza ukurasani Kwake X

Mlale Unono 😄
Soon utasikia Tanzania imewezesha
 
Hiyo taarifa ya mnyika kwenda Senegal hiyo Novemba nilishawahi kuwekwa kwenye vyombo vya habari au ndo kututengeneza kiakili.?
 
Katibu mkuu wa Chadema mh John Mnyika amesema Mapambano yamewezesha mh Faye kushinda Uchaguzi wa Rais Senegal

Mnyika anasema November 2023 alikuwa Nchini Senegal kama sehemu ya Ujumbe kutaka kiongozi wa Upinzani mh Sonko na mwenzake waachiwe Huru

Mnyika ameeleza ukurasani Kwake X

Mlale Unono 😄
Toba, I smell a stinking fish...Kama alikwenda Kusaidia then anatupa taarifa Kuna a force behind this change...Pengine mabeberu Wana recruit new agents...Nimewaza tu mwenzenu kwakua vyama vyetu vina support ya Hawa ma bwana badala ya kujisimamia vyenyewe
 
...Ujumbe kutaka kiongozi wa Upinzani...
Unajisikiaje Raha kujiita Mpizani badala ya kujiita Mshindani? Neno Upinzani limebeba "negative energy" na neno Mshindani limebeba "Positive Energy".

Badilikeni Enyi wanasiasa kama mnania njema na Maendeleo ya Taifa la Tanzania na watu wake. Ujumbe huu aupokee Mnyika na Wenzake.
 
Hayo mapambano fanyeni na hapa Tanzania, ila CDM sijui lini watapata akili..!!
 
Rais aliyetoka nayeye alikuwa mpinzani ila, ghafla akataka kuinajisi Katiba, ngoja tuone wengi waafrica wanaingia ikulu very humble ila wakionja madaraka wanageuka na kusahau movement zote
Watu weusi hawawezi kujiongoza wala kuongoza wengine

Ni jamii Masikini, Dhaifu na hovyo wasiopendana na wanaochukia maendeleo ya wenzao
 
Yaani CHADEMA maongo maongo na matapeli ya kisiasa.ndio maana chama kimedumaa utafikiri ndama aliyekosa maziwa.
Ccm ndiyo imedumaa. Chama gani kinatawala zaidi ya miaka 50 na serikali yake hakiwezi kujenga matundu ya vyoo?
 
Wananchi ndio wenye funguo za mabadiliko, viongozi wa upinzani ni wasimamizi tu wa kuwezesha hayo mabadiliko, kuwalaumu wasimamizi kwa kuchelewesha mabadiliko huku sisi wenye funguo tumejifungia ndani hakuna tunachofanya ni kulea tatizo muda mrefu zaidi.

Hapo ni kura zipigwe 2025, zisimamiwe na wapiga kura wenyewe ili kuzuia wizi usitokee ndipo mabadiliko yatafanyika, lakini kukimbia hata kupiga kura zenyewe huku tukiwalaumu viongozi wa upinzani ni kutojielewa kabisa, hatujitambui.
 
Katibu mkuu wa Chadema mh John Mnyika amesema Mapambano yamewezesha mh Faye kushinda Uchaguzi wa Rais Senegal

Mnyika anasema November 2023 alikuwa Nchini Senegal kama sehemu ya Ujumbe kutaka kiongozi wa Upinzani mh Sonko na mwenzake waachiwe Huru

Mnyika ameeleza ukurasani Kwake X

Mlale Unono 😄
---
Katika ukurasa wake wa X Mnyika anaandika yafutatyo:

Mapambano yamewezesha Bassirou #Diomaye Faye (44) kushinda uchaguzi wa urais kwenye vituo vingi #SenegalElections .

Mwezi Novemba 2023 nilikuwa #Senegal kama sehemu ya ujumbe wa kutaka Kiongozi wa Upinzani Ousmane Sonko ambaye pamoja na mwenzake Diomaye waachiwe huru na chao Chao cha #PASTEF ambacho wakati huo kimefutwa na Serikali kirejeshwe na wote wapewe haki ya kushiriki uchaguzi wa 2024.

Nilichobaini wakati huo ni kuwa yalikuwepo mapambano toka mwaka 2021 wakati Rais Macky Sally alipoonyesha mwelekeo wa kutaka kugombea muhula wa tatu kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Uamuzi huo na ugumu wa maisha kwa wananchi, ukosefu wa ajira kwa vijana, madai ya mikataba mibovu ya mafuta na gesi, matumizi ya CFA frank na ufisadi Serikali vikawa kichocheo mapambano kupitia maandamano. Uamuzi wa Rais wa Senegal kuzima maandamano hayo kwa vyombo vya dola kuua raia, kuwaweka Sonko na wenzake gerezani na kufuta Chama chao ukaamsha mapambano zaidi na kusambaza moto wa mabadiliko kwa wadau wengi zaidi ya Chama cha PASTEF.

Mwezi Februari mwaka huu Rais Wa Senegal akataka kusogeza mbele uchaguzi, hata hivyo Baraza la Katiba la nchi hiyo likamkatalia na kuelekeza uchaguzi ufanyike kabla ya muhula wake kuisha tarehe 2 Aprili 2024. Uamuzi huo ilitanguliwa na maandamano mengine ya umma kupinga uamuzi wa Rais na kutaka uchaguzi ufanyike sanjari na wafungwa wa kisiasa kuachiwa huru.

Rais akalazimika kufanya mambo mawili kwa haraka: kutangaza uchaguzi na kupeleka Bungeni amnesty bill.

Hapo ndio ikaendelea safari ya mapambano kwa #OusmaneSonko na #Diomaye kutoka na kujitokeza kwa umma tarehe 15 Machi 2024 kuanza kampeni na hatimaye #DiomayePresident kupigiwa kura 24 Machi 2024. Imekuwa ni mapambano na kampeni ya miaka takribani mitatu kama utaanzia 2021, ama zaidi ya hiyo kama utaanzia Sonko alipogombea mara ya kwanza 2019 au wawili hao na wenzao walipounda Chama cha PASTEF 2014 baada ya kutoka Serikalini wakiwa wakaguzi wa kodi.

Mgombea wa coalition Yao iliyoundwa baada ya PASTEF kufutwa alipaswa kuwa Sonko. Hata hivyo tofauti na mwenzake ambaye alikuwa mahabusu, Sonko alishapatikana na hatia kwenye kesi kadhaa za kisiasa na mojawapo ikasababisha aondolewe kwenye orodha ya wagombea urais. Haraka akamuunga mkono mwenzake ambaye alikuwa Katibu Mkuu wake kwenye Chama. Na Bassirou D. Faye maarufu kama Diamaye akaogelea kwenye mawimbi ya mapambano na mabadiliko yaliyofunguliwa na Sonko. Ndio maana kauli mbiu ya waSenegal katika uchaguzi huu imekuwa kwa lugha yao ya kiWolof #DiomayemMooySonko yaani Diomaye ni Sonko.

Nimeshuhudia nguvu ya pamoja ya wawili hawa sio tu katika mabango, bali katika vituo vya kupigia kura nilivyotembelea jana asubuhi mpaka wakati wa matokeo jioni. Sasa kinachusubiriwa ni Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo kukamilisha mchakato wa majumuisho na kumtangaza mshindi. Mapambano yameshinda Senegali, ni vyema nchi hiyo sasa ikajifunza kwenye mapito ya Marais Wade na Sally na kizazi hiki kipya kilete mabadiliko kwenye maisha ya watu. Kwetu Tanzania tuendeleze mapambano ya kikatiba na kisheria kuwezesha chaguzi huru na haki. Tujiandae kwa #WikiYaMaandamano 22 mpaka 28 Aprili 2024.

Pia soma:
- Senagal imechagua Rais kijana kuliko nchi yoyote Africa
Matatizo yaliyopo nchi ya Senegal na kwetu yapo.
Bahati mbaya viongozi wetu hawapo tayari kurekebisha sheria kanuni na taratibu zenye kutoa haki,tunaishi kimazoea miaka nenda rudi !!
 
Sonko nae muda wake ukifika atagoma kuondoka Akili za kiafrika ni za kijinga sana.
 
Wananchi ndio wenye funguo za mabadiliko, viongozi wa upinzani ni wasimamizi tu wa kuwezesha hayo mabadiliko, kuwalaumu wasimamizi kwa kuchelewesha mabadiliko huku sisi wenye funguo tumejifungia ndani hakuna tunachofanya ni kulea tatizo muda mrefu zaidi.

Hapo ni kura zipigwe 2025, zisimamiwe na wapiga kura wenyewe ili kuzuia wizi usitokee ndipo mabadiliko yatafanyika, lakini kukimbia hata kupiga kura zenyewe huku tukiwalaumu viongozi wa upinzani ni kutojielewa kabisa, hatujitambui.
Tanzania hakuna upinzani hilo ulijue hata maandamano yana pa kuanzia na pakuishia strategic plan lazima iwepo.Viongozi wa upinzani Tanzania wanahongwa sana na wanafanya kazi ya kuchezea akili za wananchi tu.
 
Back
Top Bottom