Watakaoanzisha fujo uchaguzi wa chadema watashughulikiwa - Mnyika
- Tunachokijua
- John Mnyika ni katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Tanzania (CHADEMA), Chama hiko kwa hivi sasa kipo kwenye mchakato wa kuelekea uchaguzi mkuu ndani ya chama utakaofanyika January, 2024.
Tarehe 07-01-2025 Mnyika alifanya mkutano na waandishi wa habari tazama hapa, kueleza kuhusu kuelekea uchaguzi mkuu wa Chama hiko tarehe 21-01-2025 ambapo alielezea taratibu mbalimbali ikiwemo kuwataka wagombea kufuata maadili na kanuni za chama na kubainisha kuhusu uwepo wa wa vyombo vya habari siku ya uchaguzi.
Kumekuwepo na grafiki zinazosambaa zikiwa na utambulisho wa Jambo Tv zikidai kuwa ni kauli zilizotolewa na katibu mkuu wa Chadema alizozitoa katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika tarehe 7 January 2024.
Uhalisia wa grafiki hizo upoje?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa kauli hizo si za kweli na hazijachapishwa na Jambo Tv. Ufuatiliaji wa kimtandao umebaini pia baadhi ya mapungufu kadhaa katika grafiki hizo ikiwemo ujumbe uliopo kwenye grafiki kuwa mrefu kulinganisha na machapisho mengine ya Jambo Tv, pia kumekuwepo na makosa ya kiuandishi mathalani grafiki moja ilikuwa na maandishi na mwisho kumalizikia na kituo/nukta (.) jambo ambalo halifanyiki katika grafiki za Jambo Tv.