- Source #1
- View Source #1
Wakuu,
Je, ni kweli John Mnyika amezungumza maneno haya?
Je, ni kweli John Mnyika amezungumza maneno haya?
- Tunachokijua
- John Mnyika ni Katibu Mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).
Madai
Kupitia mtandao wa Facebook mtumiaji mmoja amechapisha grafiki yenye utambulisho wa Global TV ikiwa na ujumbe kuwa unaoleza kuwa, Katibu Mkuu wa CHADEMA amesema kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho ananufaika na kesi ya Tundu Lissu.
Uhalisia wa madai hayo ni upi?
JamiiCheck imefuatilia Taarifa hiyo na kubaini kuwa si ya kweli.
Kupitia ufuatiliaji kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu imebainika kuwa hakuna chanzo chochote cha kuaminika kilichomnukuu John Mnyika kuzungumza maneno hayo.
Ufuatiliaji zaidi umebaini kuwa Taarifa hiyo haijachapishwa na Global TV kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kama inavyoonesha grafiki hiyo yenye utambulisho wa chanzo hicho.
Pia hakuna taarifa yoyote katika mtandao wa X wa John Mnyika akitoa taarifa ya kumshutumu Heche kuwa mnufaika wa kesi ya mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu.