Mnyika: Nyimbo za MC Mwingira zitakuwa hazina ya CHADEMA

Mnyika: Nyimbo za MC Mwingira zitakuwa hazina ya CHADEMA

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema chama hicho kitamuenzi marehemu George Mwingira, maarufu kama MC Mwingira kwa kuzifanya nyimbo zake kuwa hazina ya chama hicho.

MC Mwingira alifariki dunia katika ajali ya basi la SAMA Luxury lililokuwa likisafiri kutoka Songea kuelekea Dar es Salaam, usiku wa kuamkia Jumanne, Agosti 12, 2025. Ajali hiyo imetokea katika eneo la Iyovi, mkoani Morogoro.
Akizungumza katika mazishi ya MC Mwingira yaliyofanyika katika Kijiji cha Litapwasi Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma Agosti 16, 2025, Mnyika amewataka wanachma wa CHADEMA kumuenzi na kushikamana na familia yake.


 
Back
Top Bottom