Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Katibu Mkuu wa CHADEMA leo tarehe 14, aneongea na waandishi wa habari na kuwajulisha kuhusu hali ya kuenguliwa kwa wagombea wao kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge na Udiwani.
Mnyika amesema kuwa kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali ambavyo Chadema inavyo ndani ya tume, mchezo ambao tume inafanya ni wa aina mbili:
1. kuchelewesha kutolea maamuzi ili watakaorudishwa wachelewe kampeni
2. Pili ni kupoteza muda ili kupoza hasira za umma na hatimaye ibariki vitendo vya kidhalimu vya uengua wagombea bila kuwa na sababu za Msingi
Mnyika amemuandikia barua mkurugenzi wa NEC kumtaka arudishe wagombea wote wa CHADEMA mara moja.
Pia Mnyika ameendelea kuuumbusha umma kuwa matendo haya hovyo ya tume yanatokana na kuwa tume imejaa makada wa CCM kama vile mkurugenzi, na akauonya umma kuwa leo utambue sababu za kutaka tume huru ya uchaguzi.
Kwa habari zaidi, msikilize Mnyika hapa: