Uchaguzi 2020 Mnyika: Tume ya Taifa ya Uchaguzi inashiriki mchezo wa kuvuruga Uchaguzi

Uchaguzi 2020 Mnyika: Tume ya Taifa ya Uchaguzi inashiriki mchezo wa kuvuruga Uchaguzi

Kwa hiyo hamtaki kufuata sheria kwenye kutekeleza wajibu unao wahusu. Sasa kwa akili za kawaida nani hasa hapa anataka kuanzisha vurugu kati ya CHADEMA kupitia katibu wake Mnyika na NEC!

Halafu bado mnang'ang'ana majukwaani eti watanzania wawaamini! Watanzania waleo wanapima kwa vigezo vyote nani wa kumkabidhi madaraka kwa kutafakari kwa makini kabisa. Watanzania ninawaamini hawawezi kufanya makosa.
Hawa Ndugu Bureeee kabisa yani. Wao wanachojua ni uongo uongo tu!
Hamna mgombea zaidi ya utapeli hapo
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA leo tarehe 14, aneongea na waandishi wa habari na kuwajulisha kuhusu hali ya kuenguliwa kwa wagombea wao kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge na Udiwani.​

Mnyika amesema kuwa kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali ambavyo Chadema inavyo ndani ya tume, mchezo ambao tume inafanya ni wa aina mbili:
1. kuchelewesha kutolea maamuzi ili watakaorudishwa wachelewe kampeni

2. Pili ni kupoteza muda ili kupoza hasira za umma na hatimaye ibariki vitendo vya kidhalimu vya uengua wagombea bila kuwa na sababu za Msingi

Mnyika amemuandikia barua mkurugenzi wa NEC kumtaka arudishe wagombea wote wa CHADEMA mara moja.

Pia Mnyika ameendelea kuuumbusha umma kuwa matendo haya hovyo ya tume yanatokana na kuwa tume imejaa makada wa CCM kama vile mkurugenzi, na akauonya umma kuwa leo utambue sababu za kutaka tume huru ya uchaguzi.

Kwa habari zaidi, msikilize Mnyika hapa:

Wewe Bwana acha Uongoo!
NEC haiamuliwi mambo yake na mtu wala Chama.
Mnyika ni nani aiagize NEC?
 
Kuna watu wanaongea vitu wasivyovijua kuhusu TUME, kuthibisha hilo naomba ajitokeze wa kueleza kura zinaweza kuibiwa vip katika mchakato wa kupiga na kuhesabu kura?
 
Kwahyo Mnyika unataka kutuambia kuwa Wagombea wanaorudshwa kwenye kinyang'anyiro ni kwa sababu umemuandkia Mkurugenzi NEC barua. Tume inafata sheria kwahyo utaratibu wa kushughulikia rufaa upo kisheria..!
 
Kwa jinsi mchakato wa Uchaguzi ulivyo sioni kama unashida, maana kuna chama kimesema nacho kina Makada ndani ya TUME 😀


Hicho chama kilichosema hivyo ni chama gani wakati Tume imechaguliwa na Mgombea kutoka CCM ??
 
Hicho chama kilichosema hivyo ni chama gani wakati Tume imechaguliwa na Mgombea kutoka CCM ??
Point of correction, sio Mgombea wa CCM ni Rais wa JMT na kwa nyongeza tu Tume inafanya kazi kwa Mujibu wa Sheria, Kanuni na Miongozo ambayo vyama vyote vya siasa vilishirikishwa.
 
Point of correction, sio Mgombea wa CCM ni Rais wa JMT na kwa nyongeza tu Tume inafanya kazi kwa Mujibu wa Sheria, Kanuni na Miongozo ambayo vyama vyote vya siasa vilishirikishwa.


Kumbe Mgombea wa CCM si Rais wa TZ ??
 
Back
Top Bottom