Uchaguzi 2020 Mnyika: Tume ya Taifa ya Uchaguzi inashiriki mchezo wa kuvuruga Uchaguzi

Swala sio Chama fulani, swala ni kwamba unauwezo wa kuipeleka nje ya nchi familia yako machafuko yakitokea?

Hayo machafuko yatakapotokea, unadhani watakao ikimbia nchi ni mimi na familia yangu au ni nyinyi wahujumu uchumi wa ccm!
 
Kumbe Mgombea wa CCM si Rais wa TZ ??
Gavana mbona tulikua tunaenda vizuri sasa umeanza kuharibu tena kwa kuuliza maswali ambayo hayana maana?.
Kwa msaada tu naomba rejelea Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT ya mwaka 1977.
 
Gavana mbona tulikua tunaenda vizuri sasa umeanza kuharibu tena kwa kuuliza maswali ambayo hayana maana?.
Kwa msaada tu naomba rejelea Ibara ya 74 ya Katiba ya JMT ya mwaka 1977.

Jibu swali kwanza

Kumbe Mgombea wa CCM si Rais wa TZ ??
 
Hayo machafuko yatakapotokea, unadhani watakao ikimbia nchi ni mimi na familia yangu au ni nyinyi wahujumu uchumi wa ccm!
Tate Mkuu huyajui machafuko yale yana athari kila upande bila kujali mlengo wa Chama. Ni ushauri wangu kwako kuilinda hii amani siasa isitufanye mimi na wewe kutazamana kwa namna ya tofauti.
 
Tate Mkuu huyajui machafuko yale yana athari kila upande bila kujali mlengo wa Chama. Ni ushauri wangu kwako kuilinda hii amani siasa isitufanye mimi na wewe kutazamana kwa namna ya tofauti.

Hakuna Mtanzania nikiwemo mimi, asiyependa amani. Tunachotaka ni serikali kutenda haki kwa raia wote. Ukosefu wa haki unaofanywa na serikali ya ccm ndiyo unaotufanya wapenda mabadiliko tuiombee njaa.
 
Hapa sikubaliani na wewe kiongozi manake wewe Kama kiongozi unasema mambo ambayo hata uthibitisho huna napata mashaka na maandalizi yenu ya kampeni kila siku tunaona kwenye vyombo vya habari ikitoa taarifa za rufaa ambazo zimefanyiwa kazi. Kimsingi Tume inafanya kazi kwa kufuata Sheria na zile rufaa zinafuata mchakato wa kisheria sasa ukitaka Tume ifanye kazi kwa mihemko na vitisho Kama za kwako Kuna wagombea hawatatendewa haki na mtaanza kulalamika ingekua Tume wametulia tu hawafanyi kazi sawa lakini sisi wananchi tunafuatilia kila siku tunaona Tume inatoa taarifa za rufaa. Usikaririshe wanachama wenu kulalamika hata pasipo na hoja zenye mashiko kwa kweli mnyonge mnyongeni haki yake mpeni Tume inapambana labda Kama ungekua na busara ungewashauri positively sio kudanganya kuwa eti Tume ina mpango wa kuvuruga uchaguzi wakati mpaka sasa mchakato unaoendelea ni kazi nzuri iliyofanywa na Tume.
 
Sasa jamani Uchaguzi ukiendeshwa wanavyotaka kwamba mgombea hana sifa hajui kusoma wala kuandika, hajui kuandika hata tarehe yake ya kuzaliwa, huo utakua Uchaguzi au mkutano wa Chadema maana tunajua huko Chadena tunajua anachosema mzee wa Bilicanas hakipingwi.

Ila binafsi sishangai kwa sababu Chadema nyinyi mnataka hii nchi iparaganyike wafadhili wenu wapate pa kuingilia

Sisi watanzania hatuko tayari kuigeuza nchi yetu kuwa kichaka cha mabeberu kufanya yao. Mnyika nenda Libya kama unataka kuichafua Tanzania na uiache NEC ifanye majukumu yake kwa mujibu wa Sheria wewe kama hutaki kufuata Sheria tuachie nchi yetu.
 
Hakuna Mtanzania nikiwemo mimi, asiyependa amani. Tunachotaka ni serikali kutenda haki kwa raia wote. Ukosefu wa haki unaofanywa na serikali ya ccm ndiyo unaotufanya wapenda mabadiliko tuiombee njaa.
Thibitisheni malalamiko yenu kwani mahakama hamzioni?
 
xng hua

Wewe Uvccm uwe makini! Utaweka mpira kwapani muda si mrefu. Waulize wakubwa zako watakwambia.
 
Kwanza Mnyika anasema amepata habari kutoka kwenye vyanzo vyake ndani ya Tume, unadhani hivyo vyanzo sio makada wa Chadema? Kwa hiyo mimi hapo naweza kusema kwamba Tume ina makada wa Chadema, unadhani nitakuwa nakosea? Je kama yeye ana watu wake na anaona ni sawa wakiwa ndani ya Tume, kwanini analalamikia wale anaowahisi kwamba ni ma kada wa upande wa pili? Two wrongs don't make a right. Halafu Mnyika asitake kuwafanya watu wajinga, yani huwezi kusema eti warudishwe wote regardless kwamba hawana sifa? Hilo haliwezi kutokea na kwa taarifa yake Uchaguzi utaisha na amani ya nchi hii itaendelea kuwepo.
 
Huyo Kada wao hapo NEC asituharibie Tanzania yetu, Tanzania ni nchi ya watu 50m, watu wachache wasituletee uharibifu
 
LOGIC!!!
Nchi yetu ina watu wenye akili zao na ina viazi yani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…