Habarindiyohiyo
JF-Expert Member
- Aug 11, 2008
- 263
- 16
Jamaa mshamba kweli. Anaulizwa na Diva kama ana girlfriend anajibu ooh maswala ya siasa yasichanganywe na siasa. Clouds wakaamua kumkatia simu. Yaani huyu jamaa anafikiri kila sehemu ni kuuza siasa tu? Hajui hata Obama mwenyewe huwa anahojiwa na Alex Blastick, yule mcheza filamu za ngono? Huu ushamba huu wee Mnyika.
Mtangazaji mahiri na maarufu wa kipindi cha Ala za Roho kinachorushwa na Clouds Fm ametoa siri kuhusu mahojiano yake na Mnyika. Siri hizo ni pamoja na ushamba wa Mnyika kuingiza mambo ya umma na maji katika kipindi kinachohusu mapenzi. Diva amesema pia Mnyika alitambua kwamba Diva alikasirika na kumkatia simu baada ya kukaa kujibu swali rahisi kabisa kuhusu mapenzi.
Diva ametoa sauti ya mahojiano yake hayo aliyoyafanya na Mnyika baada ya kumpigia simu na kumrekodi akimuuliza iwapo ana Girl Friend ambapo Mnyika alikataa kujibu wa kisingizio kuwa masuala yake binafsi sio ya kuyazungumza kwenye vyombo vya habari bali mambo ya umma pekee ndiyo anayoweza kuyatolea kauli kwenye vyombo vya habari.
Madai hayo yanasikika kupitia: DIVA VS MNYIKA by DivaAKAmimi on SoundCloud - Create, record and share your sounds for free
Mnyika alitoa madai hayo huku akitambua kwamba yeye ni mwanasiasa hivyo maisha yake binafsi yanapaswa kujulikane yote kwa umma bila kuficha kitu chochote.
Hali hiyo ilimfanya Diva achukie na kukata simu bila mahojiano hayo kwa njia ya simu kukamilika, hali ambayo ilimfanya Mnyika atambue kama anavyosikika kupitia: DIVA VS MNYIKA- BEHIND THE SCENE by DivaAKAmimi on SoundCloud - Create, record and share your sounds for free
..........ndiyohiyo